BREAKING
  • FANGASI UKENI

    Pata suluhisho la tatizo la fangasi ukeni pamoja na ushauri utakaokufanya uwe salama daima

  • TIBA YA NGUVU ZA KIUME

    Okoa nyumba yako kwa kupata dawa itakayo ongeza nguvu zako za kiume na kudumisha unyumba daima

  • SULUHISHO LA U.T.I

    Je hauna ufahamu wowote kuhusu U.T.I ?Je Unakabiliwa na tatizo la U.T.I?Wasiliana nami nikujuze zaidi huenda una tatizo la U.T.I lakini haujijui,na kama unalo basi tiba yake ipo

  • TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

    Je Umesumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu pasina kupata suluhisho,wasiliana nami nikupatie dawa itakayoondoa tatizo lako kabisa

BannerFans.com

Jumamosi, 13 Mei 2017

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE NA SULUHISHO LAKE

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE NA SULUHISHO LAKE






KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji
Naam ni jambo la kumshukuru Allah kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Allah kwa kila kitu katika maisha yako
Ama baada ya salam Leo ni vyema tukapata darasa kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu

Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.


Kuvimba Tezi Dume (BPH)


Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.


BPH husababishwa na nini?

Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.

Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika

damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye

kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

Dalili za BPH
Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

Hukojoa mkojo unaokatika katika
Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
Husita kabla ya kuanza kukojoa
Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH


Madhara ya BPH
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na


Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
Madhara katika figo au kibofu
Shinikizo la damu
Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
Maambukizi mbalimbali
Nimonia (Pneumonia)
Damu kuganda
Uhanithi
Vipimo na Uchunguzi

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake
kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
Matibabu

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa njia ya dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).
Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa


Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo

Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwaKula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.[Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.

Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta

hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji
Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.


Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.Kutoa mbegu (Ejaculation):

Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra

karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia

kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa mojaIngawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kwa mwezi


Prostasure Capsule




Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata vifuatavyo
Extractum of Radix Rehmanniae, Rhizoma Anemarrhenae, Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus Ligustri Lucidi, Harba Plantaginis, Radix Paeoniae Rubra.

KAZI NA FAIDA YA HII DAWA
Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la tezi dume na inawafaa Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya kujikinga na tezi dume

 Prostasure Inasaidiaje?
Dawa hii inazuia na kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume kama, kukojoa kila mara, mkojo kutoka kwa shida au maumivu wakati wa kukojoa. Prostasure inaboresha mzunguko wa damu na kuzuia ukuaji wa vijidudu wadogo wanaoweza kusababisha maambukizi katika tezi dume

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

Ijumaa, 14 Aprili 2017

FAHAMU MTI WA PINE POLLEN NA MAAJABU YAKE KATIKA KUPONYA MWILI WA MWANADAMU

MTI WA PINE POLLEN NA MAAJABU YAKE KATIKA MWILI WA MWANADAMU


Pollen pini ni poleni ya miti iitwayo chinese red pine au chinese  pine
miti ambayo huishi miaka mingi sana. Miti hii huishi hadi miaka inayofikia 1000, tabia yao kuu Ikiwa ni kuhimili mashambulizi ya wadudu, baridi na ardhi chakavu.
Hii ni miti ya kijani ya kudumu.
Chanzo cha maisha marefu ya miti hii ni poleni (pollen). Poleni ya miti hii ina uwingi wa elementi zenye faida, ikiwa ni pamoja na virutubisho zaidi ya 200. Mti huu huitwa "King Of All Pollens."
Kuna aina 22 za tindikali za amino (Amino Acids), aina 14 ya vitamini na madini adimu (trace Minerals) zaidi ya 30 na kiasi kikubwa cha kimeng'enya kinachovunjavunja protini (protease), flavonoid n.k.
Rutin (aina ya sukari) iliyopo ndani ya pine pollen ni kitu kilicho adimu sana. Hufanya kazi ikishirikiana na flavonoid na lecithin katika kuilinda mishipa ya damu ya binadamu. Protini iliyopo katika pine poleni huwa katika mfumo wa tindikali ya amino huru (free amino acid), uwingi wake ukiwa kati ya mara 5-7 ya protini ipatikanayo kutoka kwenye maziwa au mayai. Uwingi wa VC ni zaidi maradufu ya ule wa kwenye matunda au mboga mbichi za majani. Kwa sababu hiyo, Pine Pollen huitwa "The King Of Natural Vitamins".

FAIDA  ZA PINE POLLEN:


Pine Pollen ni namna ya chakula cha ziada cha kutunza afya chenye ufanisi wa hali ya juu. Inaweza kukuondolea uchovu haraka, kukuongezea nguvu, kupunguza tatizo la kukosa choo, kuboresha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kutunza uimara wa ngozi na kuifanya ivutie, kukufanya uwe na furaha na mwenye nguvu na kuboresha kumbukumbu.
Sasa hivi, pine pollen imeshajizolea umaarufu katika nchi nyingi kama majani muhimu kwa afya. Sababu kubwa ni kuwa pine pollen inahuishwa na kuishi maisha marefu. Hukupa mtumiaji chakula kilichojitosheleza.
Madini adimu katika pine pollen, flavonoid, arginine ,VC, VE, B-carotene na selenium vinaweza kuondoa radikali huru kwa kuboresha ufanyaji kazi wa SOD na kuzuia lipid peroxide, kuondoa alama za umri (Age spots), na kupunguza kasi ya kuzeeka kwa seli.

KUONDOA UCHOVU:
Pine pollen si kwamba ina uwezo wa kukupa virutubisho moja kwa moja tu bali kukupa

nguvu na kuongeza ustahimilivu wako dhidi ya uchovu kwa kuboresha mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula. Pine pollen inaweza kurekebisha mfumo wako wa fahamu, kupunguza msongo wa mawazo na kuondoa uchovu.Isitoshe, pine pollen inaweza kupunguza kiwango cha tindikali ya lactic.

KUTUNZA NGOZI NA UREMBO

Pine pollen ina uwingi wa tindikali za amino, vitamini asilia na vimeng'enyo vya aina nyingi. Inaweza kuongeza ufanyaji kazi wa ngozi, kuifanya ngozi iwe ya kuvutika, na kuzuia kuzeeka kwa ngozi. VC, VE, na VB vinaweza kuungana pamoja na luamsha seli, kuondoa radikali huru, kuzuia ubadilikaji wa rangi usoni wa mwanamke mwenye mimba (chloasma), kuzuia wekundu wa ngozi chini ya macho (malar rash), kupunguza na kuzuia chunusi, kuifanya ngozi kuwa angavu na ya kupendeza.

UFANYAJI KAZI WA TUMBO

Pine pollen ina vimeng'enya na madini yayosaidia mwili karibu 100. Inaboresha mwendo wa misuli ya tumbo na utumbo mdogo wa kujifinyanga (peristalsis) na kusaidia

mmeng'enyo wa chakula, kwa ina msaada mkubwa katika kuleta hamu ya chakula na kuondoa matatizo ya kwenye tumbo. Madini ya magnesium na vitamini B6 vinaweza kuituliza misuli na kupunguza tatizo la kufunga choo.
Tindikali ya pantothenic (Pantothenic acid) iliyopo ndani ya pine pollen huulinda utando unaotoa ute ulio juu ya utumbo mdogo. Pine pollen hufanya kazi ya kukarabati utando huu wakati umeliwa na vidonda vya tumbo, kuharisha na magonjwa ya utumbo mdogo, na husaidia sana haswa pale mgonjwa anapokuwa na mzio wa dawa alizopewa au mwili kutokuwa tayari kuzipokea dawa hizo.

KULITUNZA INI

Ini ndiyo sehemu kuu ya kuhifadhi protini katika mwili. ukosefu wa protini unaweza kusababisha tatizo la uzidifu wa mafuta katika ini (fatty liver), hali ambayo inaweza kuleta makovu kwenye ini (liver cirrhosis) au kansa ya ini. Pine pollen ina uwingi wa choline, vitamini muhimu katika kuvunjavunja mafuta, ambayo inaweza kutengeneza acetylcholine. Acetylcholine inaweza kusaidia ujenzi wa phospholipid inayoweza kuzuia tatizo la kuwa na mafuta katika ini. Tindikali za amino huru katika pine pollen, na hasa methionine, zina faida kubwa katika ini. Kwa nyongeza, flavonoid ina manufaa makubwa kwa ini.
Pine pollen inaweza kuboresha utendaji kazi wa seli za ini, kurekebisha utolewaji wa nyongo, na kuzuia kujitokeza kwa matatizo ya ini. Pine pollen inaimarisha kinga za mwili, inaongeza uwezo wa ini wa kutoa sumu, na kulinda ini dhidi ya magonjwa. Kwa nyongeza, pine pollen inaweza kulilinda ini kutokana madhara ya unywaji wa pombea wa kupindukia, na ina msaada mkubwa katika ukarabati wa seli za ini zilizoharibika.

KULINDA MISHIPA YA MOYO NA UBONGO

Kiwango cha nyuzinyuzi (Fiber) katika pine pollen kinafikia hadi asilimia 29. Kwa namna moja, nyuzinyuzi zinaweza kupunguza kiwango cha chakula; kwa upande mwingine,

zinaweza kuzuia au kupunguza kasi ya ufyonwaji wa cholesterol na triglyceride. Isitoshe, pine pollen inaweza kufanya mtu asikie haja haraka na kutoa mafuta ya ziada. Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa pine pollen inaongeza kiwango cha kutolewa cholesterol kwenye kinyesi mara 0.8, triglyceride kwa asilimia 200, na aina zaidi ya kumi ya mafuta kwa silimia 700.
Lecithin iliyopo ndani ya pine pollen inachochea uunguzwaji wa mafuta. magnesium inaweza kuuamsha mfumo wa vimeng'enye. Flavonoid inaweza kupunguza lipid, kama cholesterol, katika damu. Vitamini mbalimbali zinaweza kuongeza mnyumbuko wa mishipa ya damu. Rutin inaongeza kupenyeka kwa kapilari, na hivyo kuongeza mzunguko wa damu kwenye vijishipa vidogo vya kwenye moyo na ubongo. matumizi ya pine pollen yanaweza kuimarisha utendaji kazi wa mwili, kuimarisha seli za ubongo, kurekebisha mfumo wa homoni wa mwili, kupunguza lipid ndani ya damu, kuzuia na kusaidia tiba za magonjwa ya mishipa ya ubongo na mishipa ya moyo.

KUZUIA KANSA

Pine pollen inaweza kukupa chakula kamili kilichojitosheleza. Kwa hiyo inaweza kuzizuia seli za uvimbe zisiendelee na kuwa kansa kwa kukosa lishe kamili au kinga za mwili za kutosha. Pine pollen inaweza kuwasaidia wagonjwa kupona haraka zaidi.
Pine pollen imesheheni uwingi wa bidhaa zinazozuia kansa, kama B-carotene, vitamini E

na madini adimu kama selenium, germanium na polysaccharide, n.k.
Tiba za chemotherapy na radiotherapy zinaweza kuleta madhara makubwa kwenye mfumo wa kutengeneza chembechembe za damu, mmeng'enyo wa chakula na kinga za mwili. pine pollen inaweza kuingia ndani ya damu haraka na kuboresha kazi za kinga za mwili, na kuonda madhara mabaya ya radiotherapy na chemotherapy kama uchovu, kukosa nguvu ghafla (asthenia), kukosa hamu ya kula (anorexia), kutapika, kuharisha, matatizo ya haja ndogo, kuumwa kichwa, kukosa usingizi (insomnia), mapigo ya moyo kwenda mbio, kutoa jasho, na nywele kutoota, n.k. pine ina uwingi wa vitamini, vimeng'enya, biotin, elementi adimu na vitu vingine vya manufaa, vinavyoweza kurekebisha ufanya kazi wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kuamsha marrow ili iweze kuzalisha damu, kuongeza wa seli wa kuondoa sumu, na kukarabati viungo vilivyoharibika.

KULINDA UZITO WA MWILI

Pine pollen ina chakula kilicho kamili, chenye uwingi wa nyuzinyuzi na kalori ndogo. katika mafuta yaliyomo, asilimia 72.5 ni mafuta yasiyoganda (unsaturated fatty acids), ambayo yanaweza kufanya kazi na vitamini E katika kuweka kiwango kizuri cha cholesterol na kukufanya uwe mwembamba na mwenye umbo lenye uwiano.

MENGINEYO

Watu wenyewe matatizo ya tezi dume (prostate) wameonyesha kupata maendeleo mazuri baada ya kutumia pine pollen.
Watu wenye kisukari wanapata nguvu kwa muda mfupi sana. Wakiwa wanatumia dawa, kiwango cha sukari katika damu ya wagonjwa hushuka hadi kawaida na baadaye wanaweza kuacha kutumia dawa.
Pine pollen husaidia kutibu maumivu ya kwenye maungio ya mifupa
Pine pollen huzuia mafua na mzio (allergy)
Pine pollen huzuia kupungukiwa na chembechembe nyekundu za damu

Noted;Miti ya pine pollen haipatikani Tanzania kama nilivyosema awali kuwa inapatikana nchini china hivyo Mimi Dr Naytham Masoud kwa kushirikiana na green world company tumefanikiwa kutengeneza majani ya Chai ya pine pollen ili yaweze kutumika na kuwasaidia waishio Tanzania

MAJANI YA CHAI YA PINE POLLEN

Majani yetu haya tumeyatengeneza kwa kutumia
 (1)Pine  Pollen Extract
(11)Green Tea Powder
Pine pollen imesheheni virutubisho vingi ambavyo vinaongeza kinga za mwili na inaboresha viungo vya mwili
Husimamia tezi za homoni (endocrine system) na kuweka uwiano mzuri wa estrogen na testosterone kwa wanawake na wanaume
Hupunguza kiwango cha sukari katika mwili na kulinda mifumo ya mishipa ya moyo na ubongo
Hupunguza na kuondoa matatizo ya tezi dume.


Yafaa Kutumiwa Na:
Watu wenye upungufu wa kinga za mwili, wanaokosa hamu ya kula, wanaokosa choo, au watu wanaofanya kazi za kutumia akili
Watu wanaochoka haraka, wenye udhaifu wa mwili au akili, au wenye afya duni
Watu wenye pressure ya juu, wenye lipid kwa wingi, cholesterol nyingi, wenye mishipa ya damu iliyojaa mafuta (atherosclerosis), moyo kushindwa kufanya kazi, ukosefu wa damu ya kutosha kwenye ubongo (celebral infarction)
Watu wenye kisukari na wenye madhara ya kisukari
Watu wenye ngozi zinazozeeka
Watu wenye matatizo ya ini (kutokana na ulevi,mafuta, hepatitis)
Wanaume wenye kiwango kidogo cha mbegu au wanaokosa hamu ya kufanya mapenzi
Wanaume wenye upungufu wa testosterone

Mpendwa msomaji nashukuru kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema
 ASANTE SANA NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA  KAMA UNA MAONI\USHAURI NIANDIKIE KUPITIA NAMBA NA EMAIL ZANGU HAPO CHINI

 KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA
Naythamhealthcare.blogspot.com


Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
 E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

Jumamosi, 4 Februari 2017

SULUHISHO LA NGOZI YENYE MAFUTA

SULUHISHO LA NGOZI YENYE MAFUTA

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, alhamdulillah ni siku nyingine Allah katujaalia sifa na shukran zirudi kwake aliye juu na aliye mkuu
Naam,Leo twazungumzia ngozi yenye mafuta na suluhisho lake

NGOZI YA MAFUTA IPOJE?
Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia.
 Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa,Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mengi

Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kurithi
• Lishe mbovu
• Kuzidi kwa viwango vya  homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta

Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa na kemikali, Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.


9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

FAHAMU SABUNI YA PEARL SOAP MSAADA MKUBWA KWA WENYE NGOZI ZENYE MAFUTA

Hii ni sabuni iliyotengezwa kutokana na magamba ya viumbe wa baharini kama simbi, konokono na viumbe wengine wa baharini.
Magamba hayo yanasagwa na kutolewa Mali ghafi ya kutengeneza sabuni bora pearl soap.

*KAZI ZAKE*
~kutengeneza uzuri wa ngozi iwe na ubora wake..
~Inaimarisha uasili wa ngozi..
~Inaondoa mafuta na jasho na kuifanya ngozi kubaki kavu na safi.
~Inasafisha na inaondoa sumu ndani ya ngozi..
~Inaondoa mabaka na upele..
~Huponya muendelezo wa tishu zilizo haribika ndani ya ngozi..
~Huondoa mafuta yaliyoganda na kuziba vinyweleo na kuifanya ipumue vzr...
~Inaondoa chunusi na kuifanya sura ing'ae.
~Inang'arisha ngozi
~Inazuia uharibifu wa ngozi unaotokana na miali ya jua na miali na kemikali nyingine kupitia ngozi.
~Inaondoa mba wa shingoni, mwilini na hata kichwani,
~Inaondoa Fungus za aina zote hata kwa wanaonuka miguu wameliwa vidole wakivua viatu, .
~Inaondoa harara kwa wanaokaa maeneo ya joto kali
Ni nzuri kwa wanawake na wanaume watoto, vijana na wazee..

*MATUMIZI*
1.loweka ngozi kwa maji..
2.paka sabuni juu ya ngozi..
3.sugu kwa dakika 1-3.....
4.suuza kwa maji safi.
5.tumia mara 2 kwa siku kupata matokeo mazuri
Ina harufu nzuri na isiyoumiza pua zako,harufu salama ya maua na zabibu..

*ANGALIZO*
sabuni hii haijatengenezwa kwa kemikali za viwandani ni Tiba mbadala, hivyo unashauriwa kuitumia na kutokupaka vipodozi vya kemikali, hasa Lotion zenye hydroquinone, ina maana unatibu Kisha unajeruhi tena, Tumia Lotion zisizo na hizo kemikali.
*_Kwa Kuzipata sabuni hizi wasiliana nasi kwa kupiga au watsup no. +255623026602 kwa sh.5,000 kwa rejareja na bei ya jumla pia zinapatikana.

Jumanne, 31 Januari 2017

FAHAMU ATHARI ZA MFADHAIKO (DEPRESSION) NA SULUHISHO LAKE


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Alhamdulillah naendelea vyema nanyi pia wapenzi wasomaji wa blog hii natumaini muwazima
Naam,nina imani kila mmoja wetu ameshapata kuwa na huzuni wakati fulani, ni kitu cha kawaida kinachotokea wakati umepotelewa na kitu, kutokana na mihangaiko ya maisha au kutokana na kudharauliwa. Huzuni ikizidi na ikienda kwa siku nyingi mfululizo (wiki mbili au zaidi) na ikiambatana na hali ya kujiona kuwa si wa thamani tena, kwamba ni mtu usiye na msaada wowote  basi hii inaweza kuwa ni zaidi ya huzuni na ikawa yenye athari katika afya ya mwanadamu na hapo utakuwa umepata tatizo la kiafya mfadhaiko, ugonjwa ambao kwa bahati nzuri una tiba.

MFADHAIKO(DEPRESSION)
Ni ugonjwa unasababisha mtu kuwa na huzuni kila wakati na kukosa hamu ya kufanya vitu au kutenda yale aliyopenda sana kufanya zamani. Mfadhaiko ni ugonjwa unaoathiri namna mtu anavyojisikia, anavyofikiri na tabia yake.

CHANZO CHA MFADHAIKO(DEPRESSION)

Chanzo halisi cha ugonjwa huu mpaka sasa bado hakijafahamika Wataalamu wanasema kuwa ni muunganiko wa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na urithi, mazingira ya maisha, mambo ambayo mtu amekutana nayo katika maisha na sababu za kisaikolojia.
Mtu anaweza kukutana na jambo moja tu kubwa na baya katika maisha yake kama kufiwa na mtu wa karibu, mahusiano mabaya ya ndoa au kubakwa na akapata mfadhaiko.
Mtu mwenye mfadhaiko hupungukiwa na uwezo wake wa kutenda kazi kiasi kwamba yeye na walio karibu naye wote huathirika.

Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa ya kulevya. Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wenye magonjwa ya moyo, waliopatwa na kiharusi, wenye kansa, kisukari, ugonjwa wa Parkinson’s na baadhi ya magonjwa mengine huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na mfadhaiko.
 Mtu mwenye mfadhaiko pamoja na magonjwa hayo mengine huwa kwenye hali mabaya zaidi ya kiafya na hupata shida zaidi kuutibu ugonjwa huu.

Utafiti wa zamani ulisema kuwa watu wenye matatizo ya mfadhaiko waliathirika kutokana na kutengwa na jamii, lakini utafiti wa hivi karibuni umetoa majibu tofauti na kuonyesha kwamba mtu anatengwa na jamii kutokana na mfadhaiko alio nao.

Mfadhaiko ni ugonjwa ambao umefahamika toka zamani sana. Ndugu Hippocrates aliuita ugonjwa huu Melancholia.

Watu wengi mashuhuri wameumwa ugonjwa huu na wengine katika maisha yao yote.
Abraham Lincoln, raisi wa 16 wa Marekani na Winston Churchil wa Uingereza ni baadhi ya watu walioumwa ugonjwa huu katika maisha yao yote.

AINA ZA MFADHAIKO(DEPRESSION)
Tatizo hili la kuwa na mfadhaiko linakuja kwa namna nyingi. Hapa chini ni baadhi ya aina za mfadhaiko

MAJOR DEPRESSIVE DISORDER (MAJOR DEPRESSION)

Mgonjwa mwenye aina hii ya mfadhaiko anakuwa na mchaganyiko wa dalili nyingi za mfadhaiko ambazo zitamfanya ashindwe kulala, kusoma, kufanya kazi, kula na kufaidi vitu ambavyo awali vilikuwa vinamvutia sana.
Aina hii ya mfadhaiko humpotezea kabisa mgonjwa uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za kazi vizuri na Watu wengine hupatwa na hali hii mara moja wakati wengine hurudiwa mara nyingi zaidi

 DYSTHYMIA DISORDER(DYSTHYMIA)

Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko anaweza kuwa na ugonjwa huu kwa muda mrefu, pengine miaka kadhaa, lakini hana dalili ambazo ni kali sana kama za aina ya kwanza hapo juu.
 Mgonjwa hufanya kazi zake ingawa si kwa ufanisi mkubwa na huwa si mtu mwenye raha kamili
 Watu wengine hupatwa na hali hii mara moja tu katika maisha yao wakati wengine hurudiwa mara nyingi
Mgonjwa wa aina hii ya mfadhaiko huweza kupatwa na aina ya kwanza hapo juu mara moja au zaidi katika maisha yake.

PSYCHOTICS DEPRESSION

Endapo mfadhaiko utakuwa mkubwa na kuambatana na mtu kuwa na maluweluwe (hallucinations) na kuwa nje ya maisha halisi, mtu huyu anaweza kuwa na aina ya mfadhaiko unaoitwa Psychotic depression, ugonjwa ambao mara nyingine huitwa delusional depression.

POSTPARTUM DEPRESSION POSTNATALl DEPRESSION DEPRESSION)

Hii ni aina ya mfadhaiko ambayo Mara nyingi huwapata wanawake waliotoka kujifungua,
Kama mama mzazi atapatwa na mfadhaiko wiki chache baada ya kujifungua, anaweza kuwa amepatwa na postnatal depression.
 Wataalamu wanasema kuwa asilimia 15 hadi 20 ya akina mama hupatwa na ugonjwa huu baada ya kujifunga, bahati mbaya ni kwamba wengi hawagunduliki na wanateseka kwa miaka mingi baada ya kujifungua. Mama anaweza kuupata ugonjwa huu muda wowote katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kujifungua.

SAD (SEASONAL AFFECTIVE DISORDER)

Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu huoongezeka zaidi kadiri unavyokwenda mbali zaidi na Ikweta.
 Mwisho wa kipindi cha summer ni mwanzo wa kuona jua kwa muda mfupi zaidi au mwanzo wa saa nyingi zaidi za giza kwa siku.
 Mtu anayepatwa na mfadhaiko katika kipindi hiki huweza kuwa amepata aina hii ya ugonjwa
Ugonjwa huu hutoweka wenyewe wakati wa spring au summer.

BIPOLAR DISORDER (MANIAS  DEPRESSIVE  ILLNESS)

Aina hii ya mfadhaiko haionekani kwa wingi kama aina nyingine za hapo juu. Tabia kuu ya aina hii ya mfadhaiko ni kuwa na vipindi vya dalili kuwa juu sana na baadaye kushuka. Viwango hivi vya juu na chini huitwa manias.

DALILI ZA MFADHAIKO(DEPRESSION)

Zifuatazo ni dalili za mfadhaiko

(1)kutopenda kushirikiana na watu wengine
(2)Kuwa na huzuni kila wakati na kujiona kuwa ni mtu usiyefaa
(3)Kukosa mwamko na hamu ya kufanya shughuli/Matatizo katika kufanya maamuzi
(4)Kutotulia na kuwa na hasira
(5)Kula zaidi au pungufu ya kawaida
(6)Kulala zaidi au pungufu ya kawaida
(7)Kushindwa kutuliza mawazo kwenye jambo
(8)Matatizo ya kumbukumbu
(8)kukosa raha ya maisha
(9)Kukosa hamu ya kuanya mambo uliyoyapenda sana zamani na         hamu ya kufanya mapenzi
(10)Kujisika vibaya juu yako au kuwa mwenye makosa
(1)Kuona kwamba huwezi kutatua matatizo yako ya maisha
(12(Kuumwa kichwa kubanwa misuli, matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni, matatizo ambayo hayaponi kwa kutumia dawa
(13)Kuwa na mawazo ya kujiua

NAMNA YA KUONDOA MFADHAIKO
Mfadhaiko ni kitu ambacho kinakupunguzia nguvu zako za kufanya kazi, kinachokukatisha tamaa na hivyo kuzuia jitihada zako za kutaka kupambana na matatizo uliyo nayo.
Unaweza kuondokana na tatizo hili kwa kuwaona wataalamu wa magonjwa ya akili, kwa kutumia dawa au kupambana nalo mwenyewe. Mada ya leo ni kuhusu namna ya kuondoa mfadhaiko wewe mwenywe kwa kutumia njia ambazo hazihitaji dawa au mtaalamu; kwa kubadili staili ya maisha yako, kubadili tabia yako na kubadili namna yako ya kufikiri.

Pamoja na kuwa ni kazi kubwa kuondoa tatizo la mfadhaiko ulilo nalo, haimaanishi kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa – inawezekana, kwa kuanza taratibu na kuongeza jitihada kila siku, hata kama mfadhaiko wako ni mkubwa kiasi gani. Kupambana na mfadhaiko ni kazi inayohitaji uamuzi na kuanza kutenda wakati ambapo haupo ndani ya hali yako ya mfadhaiko. Vitu ambavyo utahitaji kuvifanya ili vikusaidie ndivyo vitu vigumu lakini ugumu wa vitu hivyo haumaanishi kwamba hutoweza kuvifanya. Itachukuwa muda kufikia kwenye hali yako nzuri ya kawaida lakini msimamo thabiti wa kutaka kukabiliana na tatizo hili utakusaidia kufanikiwa.

Utahitaji kujiwekea malengo machache na rahisi ya kuanza nayo na taratibu kujijenga kuanzia hapo. Tumia njia zote unazoweza kupata, anza na vitu vichache na kila siku hakikisha unafanya kitu fulani. Pima maendeleo yako na usikose kujipongeza pale unapopiga hatua. Hatua tutakazokupa hapa unaweza kuona kama ni ndogo na ukazibeza lakini haraka zinajijumuisha na kukupa matokeo mazuri katika kupambana na tatizo lako. Anza kwa kufanya yafuatayo:

1. JENGA MAHUSIANO YA KUSAIDIANA

Kupata msaada ni jambo ambalo litakusaidia sana katika kuondoa wingu la mfadhaiko lililoko mbele yako, peke yako itakuwa vigumu kuendelea na jitihada zako za kupambana na tataizo hili. Mfadhaiko kwa tabia yake, utakuzuia kutoka na kwenda kuomba msaada kwa watu wengine, lakini elewa kuwa kujitenga na upweke vinachangia kuukuza mfadhaiko ulio nao.

Utajisikia kuwa ni jambo gumu sana kwako kwenda kukutana na ndugu wa karibu na marafiki zako. Utaona kwako kuwa hilo ni jambo la aibu, litakalokuchosha, au kujisikia mkosefu kwa kuyavunja mahusiano ya awali, kwa taarifa yako, huu ndiyo mfadhaiko ulio nao ukifanya kazi yake. Kuwafuata jamaa zako si kuonyesha udhaifu na wala sio kuwa kero kwa wenzako. Watu wa karibu yako wanakujali na wapo tayari kusaidiana na wewe. Anza sasa, hujachelewa kamwe.

Washirikishe jamaa wa karibu: Eleza tatizo lako kwa watu unaowaamini, wafuate na zungumza nao ana kwa ana. Omba msaada wao, watakuwa tayari kukusaidia pamoja na kwamba ulijitoa nje ya mahusianao nao.

Jichanganye kwenye shughuli: Mara nyingi utakapokuwa kwenye mfadhaiko utapenda kujitenga na kubaki peke yako, hali ikizidi kubaki palepale tofauti na pale utakapochinganya kwenye shughuli za kijamii ambapo mfadhaiko wako utapungua. Jitahidi kujichanganya hata kama hufurahishwi sana na shughuli hizo. Jaribu haya machache kwa kuanza kujenga mahusiano na watu:

Zungumza na mtu mmoja kuhusu matatizo yako
Msaidie mtu mwenye matatizo
Pata chakula cha mchana au kahawa na rafiki
Kutana na umpendaye mara kwa mara
Msindikie mtu kuona tamasha au kongamano
Mpigie simu rafiki
Panga ratiba ya kupata chakula cha jioni na marafiki
Kutana na watu kwa kujiunga na masomo au michezo
Fanya matembezi
Mwone mtaalamu wa tiba ya akili au mtu wa ushauri

 2. PAMBANA NA MAWAZO HASI

Mfadhaiko hukufanya ukione kila kitu kuwa ni kibaya, wewe mwenyewe, mazingira unamoishi na mategemeo yako ya baadaye. Suluhu hapa ni kuyaondoa haya mawazo mabaya na kupandikiza badala yake mawazo mazuri.

Namna ya kuondoa mawazo hasi

Acha kiudhuru nafsi yako: Kuna mambo mengi ambayo huwa unayafikiria sana kuhusu nafsi yako. Jee, hayo mambo unayoyafikiria ni mambo ambayo ungethubutu kumsimulia mtu mwingine? Kama jibu ni hapana, acha kuihujumu nafsi yako na anza kufikiria mambo ambayo si mazito sana kuhusu nafsi yako.

Usijione kuwa wewe ndiye mkamilifu: Watu wengi wanaopata mfadhaiko ni wale ambao hujiona kuwa wao ni wakamilifu, hujiwekea viwango vikubwa sana vya maisha na pale inapotokea kuwa wanashindwa kuvifikia viwango hivyo wanaanza kujiona kuwa ni watu wasiofaa. Epuka kujipa mfadhaiko mwenyewe kwa kuacha kuwa na mawazo potofu.

Jichanganye na watu wenye mawazo mazuri: Hebu jaribu kuwatazama watu wenye mtazamo mzuri kuhusu maisha wanavyopambana na vikwazo vya maisha hata kwenye kitu kidogo tu kama vile kufika eneo fulani na kukosa sehemu ya kupaki gari. Wewe ungefanyaje hapo? Jaribu kuiga wanavyofanya hawa watu, hata kama ni kwa kujifanya tu (haitoki rohoni) na endelea kufanya hivyo hivyo, kiuchangamfu, kwenye mazingira mengine ya vikwazo.

Orodhesha mawazo mabaya yanayokujia: Kila wakati ukijiwa na wazo baya, liandike na nini kilisababisha upate wazo hilo. Wakati ambapo kichwa chako kimetulia, pitia mawazo haya na yajadili kama ni kweli yalifaa kuwaziwa. Litazame wazo lako kwa mtazamo mwingine tofauti; mpenzi wako kakuudhi, ukaamua kuwa huo ulikuwa mwisho wa mahusiano yenu, jee haiwezekani, kwa mfano, kuwa mwenzio alikuwa kwenye wakati wake mbaya?



3. LEA MWILI WAKO VYEMA

Ili kuudhibiti mfadhaiko ni lazima uulee mwili wako, ikimaanisha kuwa na mtindo wa maisha unaofaa, kujua namna ya kuudhiti mafadhaiko, kujua viwango vinavyoweza kufikiwa na mwili wako na kuweka kwenye ratiba muda wa kuuburudisha mwili wako.

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha: Mfadhaiko kwa kawaida huendana na matatizo ya usingizi, unaweza kulala kupita kiasi au ukakosa usingizi. Vyote ni vibaya kwako. Tafata njia za kupata usingizi kwa muda wa saa 8 kwa siku.

Pata muda wa kukaa nje kila siku:Kukosa mwanga wa jua kunaweza kuifanya hali yako ya kuwa na mfadhaiko kuongezeka. Fanya matembezi nje, pata kahawa yako nje, kaa katika bustani n.k. Lenga kupata angalau dakika 15 za kukaa juani kila siku.
Kuwa makini na msongo wa mawazo:Msongo wa mawazo unaongeza muda wa kuwa na mfadhaiko, unaongeza ukubwa wa mfadhaiko na kusababisha mfadhaiko. Vichunguze vitu vyote vinavyokusababishia msongo wa mawazo, kazi nyingi, mahusiano ya kijamii, matatizo ya kiafya n.k. kisha weka mipango ya kukwepa vyanzo hivyo
Mazoezi ya kupumzisha mwili: Kuwa na ratiba ya kila siku ya mazoezi ya kupumzisha mwili kunaweza kuondoa mfadhaiko. Jaribu vitu kama yoga, meditation, deep breething n.k.

4. FANYA MAZOEZI KILA WAKATI

Unapokuwa na mfadhaiko, mazoezi ni kitu cha mwisho ambacho mwili utapenda kufanya, lakini mazoezi ni kitu chenye nguvu sana katika kuondoa mfadhaiko. Utafiti umeonyesha kuwa mazoezi yana nguvu sawa na dawa za kuondoa mawazo. Sababu kamili haijaeleweka, lakini fikra moja ni kwamba mazoezi yanawezesha uzalishaji wa seli mpya katika ubongo

Jiwekee ratiba ya mazoezi ya nusu saa kila siku ukianza na mazoezi laini au mazoezi mazito kidogo kwa dakika kumi. Unaweza kufanya yafuatayo:

Panda ngazi badala ya kutumia lifti
Paki gari yako kwenye sehemu iliyo mbali kuliko zote
Tafuta rafiki wa kufanya naye mazoezi
Tembea wakati unazungumza na simu

 5. KULA CHAKULA BORA
Chakula unachokula kina uhusiano na namna utakavyojisikia kimwili. Hakikisha unapata mlo kamili wenye protini isiyo na mafuta sana, chakula chenye wanga, matunda na mboga. Punguza matumizi ya kahawa, pombe na chakula kilichosindikwa kwa kemikali.

Usiruke milo: Kukaa muda mrefu bila kupata kitu cho chote kunaweza kukufanya ukose raha na kuwa mchovu, jaribu kula kitu fulani kila baada ya saa 3 au 4.

Punguza sukari na chakula kilichokobolewa: Chakula chenye sukari kwa wingi, kama vile vitu vidogo vidogo vya kutafuna (snacks) na pasta, vinaburudisha kwa muda mfupi lakini baadaye vinakusababishia kuingia kwenye hali ya fikra na kukupunguzia nguvu za mwili.

Tumia vitamini B: Upungufu wa vitamini B kama folic acid au B12 unaweza kusababisha mfadhaiko. Tumia vidonge vya vitamini B-complex au ipate vitamini hiyo kutoka kwenye matunda, mboga za majani, maharage, nyama ya kuku na mayai.
Tumia chakula chenye viini-lishe kwa wingi kama ndizi (magnesium kupunguza wasiwasi, vitamini B6 kukupa umakini, tryptophan kuongeza kiwango cha serotonin), spinach (magnesium, folate kupunguza hali ya kuhangaika na kukupa usingizi) na brown rice (serotonin, thiamine).

Omega-3 fatty acids: Chakula chenye Omega-3 fatty acids hukufanya ujisike vizuri. Chanzo cha Omega-3 fatty acids ni samaki wenye mafuta (salmon, sardines n.k.).

6. TAFUTA MSAADA WA KUONDOA MFADHAIKO

Kama mfadhaiko wako unazidi kuwa mbaya, omba msaada kutoka kwa wataalamu, kufanya hivyo si dalili ya udhaifu. Mawazo chanya unayoyapata kutokana na mfadhaiko wako yanaweza kukufanya ukajioona kuwa wewe sasa ndio umefika mwisho, kwamba huna ujanja tena wa kujinasua. Kumbuka kuwa mfadhaiko ni ugonjwa tu, na unatibika. Zingatia dondoo za hapo juu kuhusu kujisaidia kupambana na mfadhaiko hata kama utapata ushauri wa kitaalamu kwani zitakusaidia uondokane na mfadahiko mapema zaidi na kusaidia ugonjwa huu usirudie tena.

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

Jumatano, 11 Januari 2017

SULUHISHO LA TATIZO LA WANAWAKE KUOTA NDEVU NA MANYOYA(HIRSUTISM)

FAHAMU TATIZO LA WANAWAKE KUOTA NDEVU NA MANYOYA(HIRSUTISM}

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji
Naam ni jambo la kumshukuru Allah kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Allah kwa kila kitu katika maisha yako
Ama baada ya salam Leo ni vyema tukapata darasa kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu

HIRSUTISM NI NINI?

Ni ugonjwa ambao wanawake hupatwa na mabadiliko ya  kuotwa manyoya sehemu ambazo kikawaida wao hua hawaoti manyoya maeneo hayo
mfano ndevu kidevuni, manyoya kifuani, usoni, na mgongoni wakati mwingine manyoya magumu kama ya kiume miguuni na mikononi

Kikawaida wingi wa manyoya mwilini mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics make up lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi kama ya mwanaume hasa ndevu kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua waathirika wengi wa shida hii ni wagonjwa

DALILI ZA HIRSUTISM

Kawaida gonjwa wa hirsutism huwa na dalili za kua na manyoya mengi kama nilivyotaja hapo juu lakini pia mgonjwa huweza kua na sauti nzito kama kama mwanaume, kuota kipara, kinembe kua kikubwa, chunusi na kupungua ukubwa wa matiti

CHANZO/VISABABISHI VYA TATIZO

Kawaida mwanamke akibaleghe huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike ndio maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke hivyo homoni za kiume zikiwa nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu ambazo hazihusiki kama nilivyotaja hapo juu
 lakini pamoja na hali hii ugonjwa huu una vyanzo vingine kama vifuatavyo.

POLYCYSTIC OVARY SYNDROME: huu ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano sawa wa homoni za mwanamke kitaalamu kama homornal imbalance hivyo mwanamke hupata mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba,  kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari za kutengeneza mayai yake.

MATUMIZI YA DAWA NA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI
hii huenda ndio ikawa chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na manyoya  kwa tabia ya kutumia dawa fulani bila maelekezo ya daktari pia siku hizi kuna maduka ya urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari  sana kiafya kwa watumiaji. kuna dawa kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na utengenezaji wa homoni{ adrenal gland] hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake mfano predinisolone vidonge na cream, sonaderm, candiderm,gentaline c, na dawa zingine zote zenye mchanganyiko huu kwani zipo nyingi ila mchanganyiko ni uleule ila majina tofauti ya viwanda. Dawa hizi hutakiwa zitumike kwa angalau wiki moja tu kutibu ugonjwa wa ngozi lakini wengine wamezigeuza kama mafuta ya kujipaka hivyo kama na wewe unapaka hizo aina za dawa ujue ndevu ziko njiani.

UVIMBE WA KANSA
kansa za kiungo hichi kilichopo juu ya figo[adrenal gland] huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na manyoya magumu ya mwili.

CONGENITAL ADRENAL HYPERPLASIA:
huu ni ugonjwa wa adrenal gland ambao mtu huzaliwa nao na kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya mengi mwilini..

CUSHING SYNDROME:
hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa zenye homoni ya  cortisol mwilini mwake kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge  kwa wagonjwa wa allergy na asthma.

Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi

VIPIMO:

Mgonjwa anashauriwa kupima kipimo kuangalia wingi wa homoni mwilini wake hasa testosterone kama zitakua zipo juu Au kupiga picha ya ultrasound ya ovary kuangalia kama kuna tatizo lolote au kupima kuangalia uvimbe wa adrenal gland  mara nyingi ni moja ya vyanzo vikuu.

MATIBABU

Mara nyingi kutafuta chanzo cha ugonjwa na kutibu ni moja ya matibabu bora zaidi lakini pale ambapo  chanzo hakionekani dawa zifuatazo zinaweza kutumika kutatua tatizo hilo

SOY CAPSULES 500MG
 hivi ni vidonge vilivyotengenezwa kiasili ambavyo husaidia sana kupanga homoni za uzazi katika hali ya kawaida na kubalance homoni,kuondoa ukavu ukeni na kuleta hamu ya tendo la ndoa pia ni msaada mkubwa kwa wenye matatizo ya uzazi

SPIRONOLACTONE;
hizi pia hutumika kuzuia homoni za kusababisha manyoya lakini ukitumia dawa hizi lazima utumie uzazi wa mpango kwani zinasababisha madhara makubwa sana kwa mtoto ikitokea  ukibeba  mimba wakati unaendelea na dozi hiyo.

DAWA YA KUPAKA YA EFLORNIRITHINE;
 Dawa ya  Eflornithine  kitaalamu hutumika kupakwa maeneo yalioathirika na nywele nyingi kuzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.

LASERS THERAPY
 hii ni miale ya mwanga ambayo inapita ndani ya ngozi kuzuia vyanzo vya ngozi{hair follicles} kuota tena mara nyingi hufanya kazi vizuri lakini gharama yake ni kubwa mno na huenda haipatikani kirahisi.



VEET CREAM :
 hii ni cream inayopatikana madukani kwa bei za kawaida ukipaka inanyoa manyoya yote japokua baada ya muda yataota tena lakini inasaidia sana hasa ukipaka mara mara kwa mara au mara moja au mbili kwa wiki.

 ELECTROLYSIS:
hii inahusisha kuweka sindano ndogo  maalumu kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza maumivu hayo.

NOTED; kama wewe ni mwanamke una ndevu au manyoya ambayo sio ya kawaida na huenda mwanzoni hayakuepo angalia kwa makini vipodozi vyako huenda ndio vinasababisha lakini pia nenda hospitali ukachunguzwe wingi wa homoni na upigwe picha ya viungo vya uzazi kama viko salama. ushauri wa bure ni kwamba serikali imekua ikipiga marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na kuvitafuta kwa magendo, ukiona kitu kimepigwa marufuku achana

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAJIFUNZE

Jumapili, 8 Januari 2017

FAHAMU SULUHISHO SAHIHI LA PUMU

FAHAMU UGONJWA WA PUMU NA TIBA YAKE

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu wote tuwazima alhamdulillah kwa nafasi ya kukutana tena hapa kupata somo la afya kuhusu ugonjwa wa pumu ambao umekuwa ukiwatesa watu sana
Naam

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya

kupitishia hewa (bronchioles tubes)hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa

nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.

MAKUNDI YA PUMU

Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;
Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.

AINA ZA UGONJWA WA PUMU

Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni 1.Pumu inayobadilika (brittle asthma):Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ta ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla(asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.2.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na

matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa(bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha. 3.Pumu

inayosababishwa na mazoezi(Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati

mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba

kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up)kabla

ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu. 4.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao.

VISABABISHI VYA PUMU

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na
Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.Magonjwa ya mapafu kamabronchitisVyanzo vya mzio(allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vile propanololwapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia auBordetella pertusis.Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuajiUpasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section):Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu

Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu
Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au mitiAtajihusisha na uvutaji sigaraAna historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familiaUtumiaji wa dawa aina yaaspirinAna msongo wa mawazoAna uambukizi wa magonjwa ya virusi kamarhinovirusMazoeziAnaishi sehemu zenye baridiAna matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)

DALILI ZA PUMU
Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na
Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)Kukohoa sana (chronic cough)hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.Kubana kwa kifua.Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.Vipimo na Uchunguzi

Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika.
Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery). Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry).Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu (Peak flow meter).X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana kama vile ugonjwa wa moyo (congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD kama vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa kama vile cystic fibrosis.Kipimo cha mzio cha ngozi(skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.

MATIBABU YA PUMU
Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya

kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo

huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa(bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia

mzio (antihistamine drugs). Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa. Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya (acute asthma)matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa(bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya

oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (intravenous muscle relaxants). Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa

hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo(mechanical ventilator). Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni

kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa. Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili(mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids), pamoja na dawa za

kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants). Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa kama influenza na pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu. Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana pumu.

DAWA MBALIMBALI UNAZOWEZA TUMIA KUTIBU PUMU

KITUNGUU THOMU

Kitunguu swaumu

Chukua punje 5 hadi 6, menya na ukate vipande vidogo vidogo lakini siyo vidogo sana na uchemshe kwenye moto na maji kikombe kimoja (robo lita), ongeza kijiko kikubwa kimoja chaasali mbichi ndani yake na uache kwenye moto kama dakika 5. Ipua na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 hadi utakapopona.



TANGAWIZI

Tangawizi

Tangawizi pia ina faida nyingi katika mwili wako na afya yako. Tengeneza juisi robo lita yenye mchanganyiko wa tangawizi, komamanga na asali. Kunywa mchanganyiko huo kutwa mara 2 au 3 kwa matokeo ya haraka.

Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya tangawizi (majimaji ya tangawizi) changanya na kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa 2 vya mbegu kavu za uwatu na uuache mchanganyiko huu kwa usiku mmoja. Kunywa mchanganyiko huu kesho yake ili kuondoa sumu kwenye mapafu yako.



MAFUTA YA MHARADALI

Mustard Oil

Chukua mafuta kidogo ya mharadali na uchanganye na kafuri (camphor) ndani yake. Jipakae mchanganyiko huu taratibu sehemu yote ya kifua mpaka uone nafuu inajitokeza. Hakikisha unayapasha mafuta kidogo katika moto kabla ya kuanza kujipaka taratibu (masaji) ili kifua kiweze kuhisi au kulipata hilo joto na hatimaye upate uponyaji kwa aharaka zaidi. Fanya zoezi hili wiki 2 hadi 3


MTINI

Mtini ni dawa nyingine ya asili (home remedy) nzuri dhidi ya pumu. Loweka baadhi ya mitini mikavu ndani ya maji kwa usiku mmoja. Kula huo mtini uliolowekwa kesho yake asubuhi kabla ya kula kitu kingine chochote. Pia kunywa maji hayo yaliyoloweka mtini kwa ajili ya kujitibu pumu au asthma. Fanya hivi kwa wiki 2 hadi 3

 CORDYCEPS PLUS CAPSULES

Availability : In Stock
Ingredients: Cordyceps sinensis mycelium, Radix ginseng

Characteristics and Benefits:

Improves immunity against attacks of microorganisms;
Possess anti-cancer property;
Enhances functions of liver, lungs and kidney;
Provides energy for those who suffer from chronic fatigue.
Suitable for:

People with compromised immunity
People with weakened functioning of liver, lungs, or kidney
People with asthma
Seniors with decreased general wellbeing
People with chronic fatigue
Athletes with increased demand

MAFUTA YA MKALITUSI

Mafuta ya mkalitusi (Eucalyptus essential oil) yanaweza kupelekea uponyaji wa haraka kwa mtu anayesumbuliwa na pumu. Weka matone machache ya mafuta haya ndani ya kikombe cha maji ya moto na usogeze pua yako karibu na mvuke unaojitokeza na uuvute ndani taratibu. Hii itasaidia kuzifungua pua zilizokuwa zimeziba sababu ya pumu na hivyo hewa inaweza kuanza kuingia na kutoka kirahisi zaidi.



ASALI

Asali

Kama unatafuta dawa ya asili ya kutibu pumu basi asali ndiyo dawa bora ya asili inayotibu pumu kuliko dawa nyingine yoyote. Unaweza kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai kilichochanganywa na robo lita ya maji ya moto walau mara 2 mpaka 3 kwa siku au unaweza kuwa unanusa ile harufu fresh ya asali mara kadhaa kila siku.

Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi changanya na nusu kijiko kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na ulambe mchanganyiko huo kila unapoenda kulala kila siku hadi upone.

KITUNGUU MAJI

Vitunguu vinajulikana kuwa na sifa ya kutibu uvimbe (inflammatory) na vimethibitika kuwa na msaada mkubwa katika kusafisha njia ya hewa. Kwahiyo kama wewe ni mhanga wa pumu au asthma basi unapaswa kuwa unatumia vitunguu maji kwa wingi kila siku vikiwa vibichi kabisa, vikiwa katika kachumbali au hata vikiwa vimepikwa pamoja namboga mboga zingine.



MATUNDA PORI NA LIMAO

Matunda kama stroberi, bluberi, papai, na machungwa yameonyesha kuwa na msaada kwa watu wanaosumbuliwa na pumu. Pia limau zina vitamin C na zinatakiwa kutumia sambamba na maji, sukari/asali na chumvi kidogo ya mawe walau mara moja kwa siku kwa majuma kadhaa ili kujitibu ugonjwa huu wa pumu.


SAMAKI

Kula mara kwa mara samaki kama ‘salmon’ (au samoni kwa Kiswahili ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu), tuna au jodari, dagaa chumvi wa baharini (sardines) kunaweza kuwa msaada mkubwa sana katika kujitibu tatizo la pumu. Samaki hawa wote huyafanya mapafu yako kuwa safi, salama na yenye nguvu katika kupambana na tatizo la pumu na kuitibu haraka na kwa ufanisi. Ingawa ikiwa hauwezi kula hawa samaki katika hali ya kupikwa basi unaweza kubadili kwa kutumia mafuta yatokanayo na samaki hawa.



ZABIBUBATA/ZABIBU NYEKUNDU

Zabibubata ni nzuri sana katika kutibu pumu. Ponda ponda zabibubata kadhaa na ongeza asali kidogo ndani yake, tumia mchanganyiko huu kila siku na ukae mbali na pumu.

KUDING PLUS TEA

Characteristics and Benefits:

Prevents common cold and flu;
Alleviates rhinitis, itching eyes, red eyes and pain in the eyes caused by wind-heat;
Detoxifies and improves healthy bowel movement;
Improves mental focus and memory;
Accelerates blood circulation, reduces blood cholesterol, blood sugar and blood pressure;
Prevent deterioration of heart and brain function;
Maintains proper body weight.
Suitable for:

All groups except for pregnant women



SHAMARI

Tumia mbegu za shamari kila mara ili kujitibu na shambulio la asthma/pumu

MAZIWA YA MOTO
Ongeza kiasi sawa cha mafuta ya mzeituni na asali ndani ya kikombe cha maziwa ya moto. Kunywa mchanganyiko huu pamoja na punje mbili au tatu za kitunguu swaumu kabla ya chakula cha asubuhi kwa majuma kadhaa. Dawa hii ya asili inaponya pumu kwa haraka sana.

MAJANI YA KOTIMIRI(PARSLEY LEAF)
Majani ya kotimiri (Parsley leaf) ni dawa mbadala nzuri sana kwa ajili ya kikohozi. Andaa chai ya majani haya na asali unywe kila siku. Itatibu kikohozi, itasafisha koo na kutibu pumu kadri siku zinavyosogea wakati ukiendelea kutumia chai hii kila siku

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAJIFUNZE

Jumamosi, 7 Januari 2017

TIBA SAHIHI YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

FAHAMU TIBA YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu mpenzi msomaji  katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote,
 Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa na  Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake,
 
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuna sababu zaidi ya 250 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume,Mtu anaweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo

MAANA YA NGUVU ZA KIUME
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.

Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za  acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi;

2. Uume kusimama kwa uregevu;

3. Kuwahi kufika kileleni;

4. Kuchelewa sana kufika kileleni ( kushindwa kufika kileleni kabisa);

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa;

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo;

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji;

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Mpendwa  msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.

Lakini nini kinachopelekea viungo hivyo vishindwe kufanya kazi vizuri?
Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia).

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua TAHADHARI kabla ya HATARI!

KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI!
Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana!

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo. Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanaume  wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana.

Nani anaweza kutibu nguvu za kiume?
Kuna watu wengi sana hivi leo wanaodai kutibu nguvu za kiume. Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kweli! Ni watu wachache sana wana uwezo wa kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Utakuta mtu anatangaza dawa ya aina moja kuwatibu watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume. Tabia hii pia imejengeka kwa baadhi ya watu, hupiga simu na kuuliza moja kwa moja, "Daktari, dawa za nguvu za kiume ni shilingi ngapi?"

 Kila mwanamume ana sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume. Kama wanaume 100 waliopungukiwa nguvu za kiume watajipanga mstari, kila mmoja atakuwa na sababu yake na chanzo chake cha kupungukiwa nguvu za kiume tofauti kabisa na mwingine.

Hii humaanisha kila mgonjwa atakuwa na dawa yake ya kipekee kabisa tofauti na mwingine. Sasa itashangaza kuona huyu kapungukiwa nguvu za kiume kutokana na mishipa ya ateri kutofanya kazi vizuri, na yule kapungukiwa nguvu kutokana na kuvimba kwa tezidume,Halafu wote wapate dawa aina moja! Hiki ndicho kinachofanyika na watu wengi wamepoteza pesa na muda kwa matibabu yasiyokuwa na maana.

Yahitajika daktari mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo, ndiye anayeweza kutibu tatizo la nguvu za kiume. Yaani, daktari ambaye anajua vizuri ndani na nje utendaji wa figo, ini, moyo n.k; awe ni daktari wa tiba asilia au daktari wa tibakemikali (yaani daktari wa hospitali) siyo kila mtu tu au kila daktari. Hata kama utakwenda kwenye hospitali kubwa yoyote duniani unayoijua, na ukagonga hodi katika chumba cha daktari, ukamwambia, "Nina tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume," atakurifaa kwa daktari maalumu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo. Hata kwa madaktari wa tiba asilia, hali ni hivyo hivyo, lazima ukutane na ambaye amebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Kwa sababu unapotibu nguvu za kiume unakuwa unatibu viungo vya mwili kwa ujumla. Daktari aliye mtaalamu anakuwa ana uwezo wa kutambua tatizo la kiungo kilichokorofisha mwilini kutokana na kumhoji mgonjwa; na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiridhisha kwa vipimo.

LISHE MUHIMU KUREJESHA NGUVU ZA KIUME
wakati mwingine mwanamme hupatwa na tatzo la Nguvu Za Kiume kutokana na kukosa madini lishe muhimu yanayohitajika mwilini mwake
Naam tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.

Antioxidant Nutrients

Upungufu wa vitamin E, vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa (sperm motility). Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa (International Units - IU) 100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza kumzalisha mwanamke (infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba mwanamke. Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye shahawa (sperm count) na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Tafiti pia zimeonyesha kwamba selenium husaidia uogeleaji wa shahawa.

Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA) ya vitamin C ni miligramu 90. Mwanaume anayevuta sigara anahitaji miligramu 125. Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits), cantaloupe, kiwi, maembe, strawberries, broccoli, cauliflower, pilipili nyekundu na juisi ya nyanya. Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source) na 22 (synthetic). Vyakula muhimu ni pamoja na ngano, karanga na jamii zake, mafuta ya mimea, mbegu zisizokobolewa (whole grains). Selenium RDA ni 15 micrograms. Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood, kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga, vitunguu swaumu.

Vitamin B12

Upungufu wa vitamin B12 hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility. Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa zake, mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).

Zinc

Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa. Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc. Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi kidogo cha homoni za kiume (low testosterone levels). Wanaume wenye shida hiyo wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba. RDA ya zinc ni miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8). Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza, dark turkey meat, lentils, ricotta cheese, tofu, yogurt, spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya. Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.

L-carnitine

Husaidia kuongeza sperm count. Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye nyama na maziwa

NOTED;KABLA YA MATUMIZI YA DAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NI VYEMA UKAWASILIANA NA DAKTARI WAKO WA KARIBU ILI KUPATA USHAURI ZAIDI

Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUNZA