Suala la kunywa maji tumekuwa tukihimizwa kila mara na
wataalamu wa Afya. Lakini zoezi hili limekuwa gumu kwa kuwa watu wengi
huona kama adhabu. Imekuwa ikihimizwa angalau kunywa Lita mbili(2) za
maji kila siku kwa kila mtu.
Nimekuwa nikiwasikia watu wengi wakidai wameenda Hospitali
kutibiwa wameambiwa wanywe maji ya kutosha ili yawasaidie. Pia wengine
wakithubutu kusema kuwa ukinywa maji mengi basi waweza tibu ugonjwa wa
UTI kirahisi kabisa. Hili ni kweli lakini tatizo watu wengi hatuwezi
kunywa hayo maji mengi.
Leo nitakupa mpangilio rahisi kabisa wa kunywa maji glass 7 kwa siku na faida zake mwilini. Hii itakusaidia zaidi maana glass 7 ni sawa na Lita 2 karibu na nusu.
Leo nitakupa mpangilio rahisi kabisa wa kunywa maji glass 7 kwa siku na faida zake mwilini. Hii itakusaidia zaidi maana glass 7 ni sawa na Lita 2 karibu na nusu.
GLASS 1. kunywa maji glass moja mara baada ya kuamka. Hii husaidia viungo vya ndani vya mwili kama figo, moyo, n.k
GLASS 1. Nusu saa kabla ya kunywa chai. Husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga asubuhi. Husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha mchana. Pia husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga jioni. Pia husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha usiku. Vilevile husaidia katika suala la mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kulala. Husaidia kuepuka kupata shambulio la moyo
Hiyo ndiyo ratiba nzuri ya kunywa maji glass 7 bila kuhangaika.
Maoni 1 :
nimeipenda hii
Chapisha Maoni