BREAKING
BannerFans.com

Jumamosi, 19 Novemba 2016

UGONJWA WA KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA/BAWASIRI (HEMORRHOIDS)

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA (HEMORRHOID) NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, sifa njema anastahiki Allah Subuhhanah'wataala Kwa afya na uzima alotujaalia,
Leo tena napenda kuzungumzia ugonjwa wa Bawasiri/hemorrhoids)
Naam watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba idadi yake inazidi kuongezeka

BAWASIRI/HEMORRHOIDS
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI
~Kuna Aina mbili za bawasiri
(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI ~hii  hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia

(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe

(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi

(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

CHANZO CHA TATIZO
~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO VIZURI
👉MATATIZO YA UMRI
👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
👉UZITO KUPITA KIASI
👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

DALILI ZA BAWASIRI
dalili za ugonjwa wa Bawasiri ni :

👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana

VIPIMO NA UCHUNGUZI
Vifuatavyo ni vipimo vinavyotumika kugundua ugonjwa wa Bawasiri
Digital rectal examination
Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

MATIBABU

Matibabu ya mwanzo ya ugonjwa huu  kawaida huwa ni ongezeko la kula chakula kilicho na faiba(high fibre) na  vinywaji Kwa wingi ili kudumisha haidresheni pia  dawa za kutibu maambukizi  husaidia kwa maumivu na mapumziko
Lakini pia kuna  Baadhi ya taratibu kubwa zinaweza kutekelezwa ikiwa dalili ni kali au hazistawi kwa mwelekeo wa matibabu ya awali
Mfano wa taratibu hizo ni :
(1)Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.

(2)Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
Coagulation (infrared, laser and bipolar)

(3)TCM MEDICAL-hapa Mgonjwa hushauriwa kutumia Dawa Aina ya TCM  kulingana na ukubwa wa tatizo Lake ambazo husaidia kurahisisha mfumo wa mmeng'enyo na kuponya chanzo cha tatizo
Mfano wa Dawa hizo ni
(1)MEAL CELLULOSE TABLET 700MG
/MEAL CELLULOSE OR DIETARY FIBER. Meal cellulose,also referred to dietary fiber,includes all parts of plant foods that the body can not digest or absorb. Therefore, it passes relatively intact through our stomach,small intestine,colon and out of our body.


(2)SPIRULINA PLUS CAPSULE 500MG
is a  natural “algae” (cyanbacteria) powder that is incredibly high in protein and a good source of antioxidants, B-vitamins and other nutrients. When harvested correctly from non-contaminated ponds and bodies of water, it is one of the most potent nutrient sources available



(3)PARASHIELD CAPSULES 500MG
(4)ALOE VERA PLUS CAPSULE 500MG

Upasuaji;
         Hemorrhoidectomy
         Stapled hemorrhoidopexy
Ni hatua ya mwisho iliyotengwa Kwa wale wanaokosa mabadiliko ingawaje sio nzuri kiafya Kwa ujumla

NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI

badilisha mfumo wako wa chakula,
Kula High fibre diet(vyakula vyenye nyuzinyuzi  kama mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.

Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)

Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa

Fanya mazoezi mepesi na sio mazoezi magumu

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI ugonjwa wa Bawasiri usipotibiwa huleta athari zifuatazo Kwa Mgonjwa
👉kupata upungufu wa damu (anemia)
👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake kwasababu husababisha maumivu Kwa Mwanamke wakati wa tendo la ndoa
👉kuathirika kisaikolojia
👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali

NOTED:
NDUGU RAFIKI KAMA UNA UGONJWA HUU EPUKA KULA NYAMA NYEKUNDU NA PILIPILI PIA UNAWEZA  WASILIANA NAMI KWA USHAURI WA MATIBABU YA KUONDOA TATIZO HILI PASIPO KUFANYA UPASUAJI
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUNZA

Hakuna maoni :