BREAKING
  • FANGASI UKENI

    Pata suluhisho la tatizo la fangasi ukeni pamoja na ushauri utakaokufanya uwe salama daima

  • TIBA YA NGUVU ZA KIUME

    Okoa nyumba yako kwa kupata dawa itakayo ongeza nguvu zako za kiume na kudumisha unyumba daima

  • SULUHISHO LA U.T.I

    Je hauna ufahamu wowote kuhusu U.T.I ?Je Unakabiliwa na tatizo la U.T.I?Wasiliana nami nikujuze zaidi huenda una tatizo la U.T.I lakini haujijui,na kama unalo basi tiba yake ipo

  • TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

    Je Umesumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu pasina kupata suluhisho,wasiliana nami nikupatie dawa itakayoondoa tatizo lako kabisa

BannerFans.com

Alhamisi, 17 Novemba 2016

TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS)

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS) LINAVYOWAANGAMIZA NA KUWAKOSESHA RAHA WANAWAKE

Asalam alaykum warhmatullah wabarakatul mpenzi msomaji wa makala hii natumaini unaendelea vizuri na majukumu ya kila siku, namshukuru Mungu kuniwezesha leo tena kuandika makala ili kukuwezesha ndugu msomaji kufahamu mambo mengi kuhusu Afya ya mwanamke na mzunguko mzuri wa hedhi, leo napenda kuzungumzia tatizo la kuvimba kwa kizazi cha mwanamke ambapo kitaalamu tunasema ni ADENOMYOSIS pia tatizo hili kwa zamani lilijulikana kama ENDOMETRIOSIS INTERNA

ADENOMYOSIS NI NINI?
~Ni tatizo ambalo nyama hutokea na kukua kama tabaka au ukuta mwingine juu ya misuli ya kizazi(ectopic glandular tissues)
~tatizo hili huwaathiri zaidi wanawake walio kati ya miaka 35_50, ingawa katika Hali isiyo ya kawaida hutokea katika umri wa chini ya miaka 35
~tatizo hili la kuvimba kwa kizazi linapotokea huambatana na damu nyingi wakati wa hedhi na kupata maumivu makali wakati wa hedhi pia maumivu huongezeka zaidi pale tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi na hivyo mwanamke mwenye tatizo hili la kuvimba kwa kizazi hupata maumivu makali chini ya tumbo ktk kitovu Muda wote pasipo kupata damu ya hedhi hata kama tarehe za kupata damu (period) zimefikia, pia damu huweza kutoka kwa wingi pia kizazi huendelea kuvimba kutokana na tabaka la ndani (basal endometrium) kujipenyeza ndani ya misuli ya kizazi na hivyo kusababisha kila siku kizazi kuendelea kukua na mwanamke kuonekana kama ana ujauzito na tumbo huwa gumu hata hivyo tatizo hili ni tofauti na tatizo la uvimbe katika kizazi (fibroids)

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUVIMBA KWA KIZAZI
~Chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijafanikiwa kuwa wazi ingawa misuli ya kizazi (uterine trauma) huchangia hili kwa kuwa huondoa ukingo wa tabaka la ndani ya kizazi kuelekea katika misuli ya kizazi pia utoaji wa mimba hovyo husababisha mirija kuchubuka pia matokeo mabaya ya uwekaji wa lupu

DALILI ZA TATIZO HILI
Dalili au viashiria vya tatizo hili ni vingi ila hata hivyo Kuna baadhi ya wanawake wenye tatizo hili hawaonyeshi dalili yoyote huku kizazi kikizid kuvimba na wengine huhisi maumivu makali ya kizazi Muda wote au wakati wa hedhi
Dalili zenyewe ni Hizi
👉chembechembe za tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi huendelea kutoa damu hivyo kusababisha damu kuvujia ndani kwa ndani Bila damu hiyo kutoka nnje
👉mwanamke huhisi uchungu wa uzazi na kuhisi kama vile anataka kujifungua kwa kuwa hupata shinikizo ukeni
👉mwanamke huhisi maumivu makali chini ya tumbo Muda wote na kila akienda katika hospital hukutwa ana uti kitu ambacho sio kweli
👉mwanamke huhisi maumivu makali zaidi kipindi cha upevushaji mayai (ovulation) au kipindi cha period (hedhi)
👉mwanamke huhisi mkojo kila wakati kutokana na kibofu kugandamizwa na shinikizo la kizazi
👉mwanamke hutoka damu kupita kiasi hadi pedi huwa hazitoshelezi pia wakati wa hedhi tumbo hubana au kukaza (abdominal eramps) Muda wote na mwanamke hutamani kuinama tu

MATIBABU NA VIPIMO
matibabu ya tatizo hili hufanyika katika kliniki Za akina mama kwenye hospital za mkoa, private na daktar hutibu kutokana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo vya MRI, ULTRASOUND na matibabu hayo huweza kuwa ya dawa za HOMONI kutegemea na ukubwa wa tatizo pia tiba nyingine ni upasuaji hasa wa kuondoa kizazi kitu ambacho hugharim sana maisha ya mahusiano iwapo mhusika hakuzaa na pia endapo mwanamke atapata tatizo hili akiwa mjamzito basi mimba Yake hutoka na hupata uchungu mapema kabla ya siku ya kujifungua

USHAURI :WANAWAKE WENGI HUWA NA DESTURI YA KUPUUZA KWENDA HOSPTAL KWA KUONA TATIZO NI DOGO HVYO NDUGU RAFIKI HAKIKISHA UNAENDA KUPIMA AFYA YAKO MARA KWA MARA ILI KUWEZA KUTAMBUA MATATIZO MAPEMA HIVYO TUACHE TABIA YA KUPUUZIA KITU HATA KAMA NI KIDOGO
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia email na namba yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA ZA AFYA TEMBELEA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email:nsalum998@gmail.com/+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI/PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)

FAHAM UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu zangu ni matumaini yangu mnaendelea vyema kabisa,napenda kuwataka radhi na kuwapa pole Kwa ukimya wangu kutokana na kupisha shughuli za uchaguzi, Nimepokea emails zenu nyingi sana za kunimiss nimefarijika napenda kuwaambia nami NIMEWAMISS NA NINAWAPENDA WOTE pamoja na hayo nimeona emails zenu zinazohusu magonjwa mbalimbali yanayowasumbua wanawake wengi na hivyo Leo hii napenda nianze na ugonjwa wa PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI )

UGONJWA WA PID NI NINI??
~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)

VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID
~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa PID zipo njia kadhaa hatarishi kusababisha maambukizi haya Nazo ni ÷
👉kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi(IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
👉Kufanya ngono isiyo salama
👉Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika
👉Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID
👉Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama

DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni
👉Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
👉Kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
👉Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
👉Kutokwa na hedhi bila mpangilio
👉kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya

VIPIMO NA MATIBABU YA UGONJWA WA PID
Matibabu ya tatizo hili yanapatikana kote nchini kwa kufata misingi ya utabibu kuzingatia majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali ili kuweza kubaini tatizo kwa kufanya vipimo tofauti
MFANO
👉FULL BLOOD PICTURE _kipimo hiki kinatumika ili kuweza kutambua aina  mbalimbali za chembe damu zilizoathiriwa na maambukizi ya PID
👉CERVICAL CULTURE_Hutumika ili kujulia aina ya vimelea waliosababisha PID
👉ULTRASOUND _hutumika kuangalia katika nyonga kama kuna athari yoyote imetokea katika mfumo wa uzazi
~mara baada ya kufanya vipimo na mgonjwa kugundulika kama ameathirika na tatizo hili mara nyingi dawa za antibiotics ambazo ni DOXYCYCLINE,CEFOXITIN,MYCIN,GENTAMYCIN,CLINDAMYCIN,SULBACTAM,AMPICILLIN, huhusika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa huu lakini ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali  ambayo imewekwa na mamlaka na wizara  ya afya kati ya sehem moja hadi nyingine hivyo si ruhusa kujinunulia dawa na kumeza pasipo ushauri wa daktari

NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na  vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉JIWEKEE TABIA YA KUFANYA VIPIMO MARA KWA MARA HASA KIZAZI
👉USIFANYE MAPENZI MARA BAADA YA KUJIFUNGUA AU MIMBA KUTOKA MPAKA UTAKAPOHAKIKISHA SHINGO YA UZAZI IMEFUNGA VEMA
👉KUWAHI KUONANA NA DAKTARI UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA
👉KUWA MSAFI NA KULA LISHE BORA
NOTED:NDUGU RAFIKI UONAPO DALILI ZA UGONJWA HUU WAHI KUPATA MATIBABU KWANI UGONJWA HUU NI MKUBWA HUWEZA KUSABABISHA UGUMBA  IKIWA HAUTAPATA TIBA VIZURI

Kwa makala zaidi za afya tembelea blog yangu hapo chini
naythamhealthcare.blogspot.com

asante kwa kuwa nami kusoma ujumbe huu rafiki kama una MAONI/MASWALI NIANDIKIE KUPITIA NAMBA NA EMAIL YANGU HAPO CHINI PIA TAFADHALI NISAIDIE KUIFIKISHA ELIMU HII KWA WENGINE

Makala hii imeandaliwa na
Dr Naytham
+255623026602/+255746465095
email;nsalum998@gmail.com
naythamhealthcare.blogspot.com
USISAHAU KULIKE,KUKOMENT NA KUSHARE NA RAFIKI ZAKO

MZUNGUKO WA HEDHI NA MATATIZO YAKE

FAHAMU KUHUSU MZUNGUKO WA HEDHI NA MATATIZO YAKE (MENSTRUATION)

Asaalam alaykum warhmatullah wabarakatul  ndugu Rafiki uliyeamua kuungana Nami kufanikisha zoezi hili la kuwasaidia wakina mama na wasichana wengi kupata elimu ili waweze kudumisha afya yao na kupata mzunguko wa hedhi ulio salama, napenda kukushukuru na kukuomba uendelee kuwa Nami kuweza kuwasaidia wakina mama na mungu atatulipa kutokana na juhudi zetu kuwasaidia wenye uhitaji

NINI MAANA YA MZUNGUKO WA HEDHI???
Ni mzunguko wa kila mwezi ambao husababisha kutokwa kwa damu kila mwezi ukeni kutokana na mimba kutotungwa,
~mzunguko wa damu umegawanyika katika maeneo makuu mawili( 1)MZUNGUKO WA DAMU UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE)
(2)MZUNGUKO WA DAMU USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE)

Napenda tufahamu kwa kina mizunguko hii
MZUNGUKO WA HEDHI UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na katika mzunguko huu mtu anaweza kupata ujauzito

MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hatoki ute ute wa Uzazi hivyo hawezi kupata ujauzito
~ pamoja na mizunguko hii miwili kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wake wa Hedhi  hapati ute ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
 pia napenda mfaham kuwa ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni (1)UTE MWEPESI
(2)UTE UNAOVUTIKA
(3)UTE MZITO
Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi na pia wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho

JINSI YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
~Kila mwezi ovari za mwanamke huzalisha yai moja ambalo Lina uwezo wa kukaa kwa muda wa masaa 36 ndani ya mirija ya Uzazi hivyo inapotokea yai hili halijarutubishwa ukuta wa mji wa Uzazi hubomoka na kutoka nje ya uke pamoja na damu  kwa neno Moja tunasema siku za hedhi,
mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza mwanamke anapoanza kupata siku zake,
Pia mzunguko wa hedhi uwe unaopevusha mayai au usiopevusha umegawanyika katika Makundi ya mizunguko mitatu yani MZUNGUKO MFUPI, MREFU NA WA KAWAIDA
~(1)MZUNGUKO MFUPI ~huu ni mzunguko wa siku 22_27
~(2)MZUNGUKO MREFU ~huu ni mzunguko wa siku 31_35
~(3)MZUNGUKO WA KAWAIDA ~huu ni mzunguko wa siku 28_30

JINSI YA KUSOMA MZUNGUKO WAKO
Tuchukulie mzunguko mfupi ambao ni siku 28
~siku ya kwanza mpaka ya tano huwa ni kipindi cha mwanamke kuingia katika mzunguko hivyo ni mwanzo wa mzunguko katika kipindi hiki ukuta wa mji wa mimba hubomoka na kutoka nnje pamoja na damu ukeni (siku ya hedhi) Katika kipindi hiki homoni za estrogen na progesterone huwa ndogo pia katika kipindi cha siku ya 6_10 ni kipindi ambacho ukuta wa Uzazi huanza kujengwa Tena kwa ajil ya kupokea kiini tete kipindi hiki mwanamke hawezi kupata mimba ila ni kipindi ambacho kinaelekea katika hatari hivyo katika kipindi hiki homoni za oestrogen huwa nyingi hivyo katika kipindi hiki yai huzalishwa (ovulation) siku ya kumi na moja ya mzunguko pia huweza kukaa kwa muda wa masaa 36 yani hutoka katika ovari na kusafiri katika mirija ya falopia mpaka siku ya kumi na nane na katika kipindi hiki homoni ya progesterone huzalishwa kwa wingi kwa ajili ya kutunza mji wa mimba pia homoni ya progesterone hupungua mwishoni mwa mzunguko yani kupungua huku husababisha mwanamke kuingia Tena katika mzunguko wa hedhi
~kipindi ambacho mwanamke ana breed hupata damu ya rangi nyekundu na huwa Ina mabonge kias kidogo na hutoka kiasi cha ML 35_50 kwa saa.
~kwa Kawaida ni kitu kizuri na cha kufurahia mwanamke kuona breed ila kutokana na matatizo wanayokutana nayo wanawake hujikuta wakichukia kuona siku zao kutokana na maumivu au adha mbalimbali wazipatazo. Ambazo ni
 (1)MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI
(2)KUKOSA HEDHI AU KUPATA KATIKA MPANGILIO USIO SAHIHI
(3)KUTOKWA NA DAMU NYINGI
Leo tuanzie hili suala la maumivu makali wakati wa hedhi na namna ya kutatua
MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI (DYSMENORHOEA)

Maumivu wakati wakati wa hedhi ni suala linalo wakumba wanawake wengi, takriban asilimia 15 ya wanawake wote duniani hupata maumivu haya wakati wa hedhi.
Maumivu haya huwa makali kiasi kwamba humunyima mwanamke uhuru wa kufanya kazi zake za kila siku.
Research zinaonesha kwa baadhi ya wanawake maumivu haya hupungua baada ya kujifungua na wengine huendelea kupata maumivu haya mpaka kikomo cha hedhi.

CHANZO CHA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Chanzo kikuu cha tatizo hili ni UWINGI WA HOMONI YA KIKE (oestrogen ), homoni hii ndio inayohusika na mfumo mzima wa mzunguko wa hedhi na inapozidi hupelekea kuongezeka kwa fat cells katika cell membrane zilizoko kwenye ukuta wa mimba (uterus) hivyo kupelekea uzalishwaji mkubwa wa chemikali ziitwazo prostaglandins.

MADHARA YA HIZI PROSTAGLANDINS
siku chache kabla ya kupata hedhi, ukuta wa ndani wa mfuko wa kizazi hutengeneza prostaglandins kwa wingi na chemikali hizi huvunjika mwanamke anapokuwa period, chemikali hizi huleta mambo yafuatayo;
1. hupunguza ukubwa wa mishipa ya damu iliyo katika mfuko wa kizazi hivyoo kupelekea misuli ya maeneo hayo kukunjana na kukakamaa na hivyo kupelekea maumivu makali wakati wa hedhi.
2. Baadhi ya chemikali hizi huingia kwenye mfumo wa damu na kupelekea mwanamke kupata kichefuchefu, kichwa kuuma, kutapika na wakati mwingine kuharisha.

NJIA HIZI ZA KUFANYA UEPUKANE NA TATIZO HILI:

1.  Tumia vyakula vyenye mafuta kidogo.
unapotumia vyakula vyenye mafuta kidogo husaidia kupunguza kiwango cha cha mafuta kitumikacho kutengeneza chemikali hizi ziitwazo prostaglandins na hivyo kukufanya uepukane na maumivu haya wakati wa hedhi.

 VYAKULA VYENYE MAFUTA KIDOGO
vyakula vyote vitokanavyo na mimea (plant based diet )
huwa na kiwango kidogo cha mafuta ikilinganishwa na vyakula vitokanavyo na wanyama kwahiyo Anza leo kutumia vyakula vitokanavyo na mimea.
lakini pia wakati wa upishi wa chakula weka mafuta kidogo katika chakula chako kuzuia uwingi wa mafuta utakaochukuliwa na mwili.

2. Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi (high fiber diet)
Vyakula hivi hutumika kupunguza na pia kubalance homoni ya kike kwani oestrogen inapotoka kwenye damu huchukuliwa na ini na baadae kupita kwenye bile duct kuelekea kwenye utumbo, na huko ndiko aina hii ya homoni ilozidi hutolewa nje ya mwili kwa kutumia nyuzinyuzi zilizoko kwenye utumbo kwahiyo unapokuwa na nyuzinyuzi  (fibers) nyingi ndivyo utaweza kukitoa kiwango kikubwa cha homoni hii iliyozidi hivyo ulaji wa vyakula vyenye nyuzinyuzi husaidia kwa kiasi kikubwa mwanamke kuepukana na tatizo hili, kwani unapokuwa na fibers chache ndivyo kiasi kikubwa cha homoni hii (oestrogen) kitakavyorudishwa mwilini.

 VYAKULA VYENYE NYUZINYUZI
vyakula vifuatavyo huwa na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi au fibers;
maharage
spinach
carrot
 mchicha
 kunde na jamii zakee
viazi vitamu
 matunda nk.

3. Epukana au tumia kidogo vyakula vitokanavyo na wananyama.
Vyakula hivi huwa na kiwango  kikubwa cha mafuta na hivyoo kupelekea utengenezaji wa prostaglandins
Lakini vyakula hivi havina nyuzinyuzi zozote hivyo hupelekea urudishwaji wa homoni hii ya kike kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye utumbo.

KWA WALIO TESEKA NA TATIZO HILI KWA MDA MREFU ANZA NA NJIA HII YA NNE,  BAADA YA HAPO ENDELEA NA HIZO TATU ZA MWANZO.

4. SOY 500MG CAPSULES
Hii ni dawa asilia kabisa iliyotengenezwa kutokana na maharage ya soy na kuwekwa kitaalam katika mfumo wa vidonge dawa hii ina homoni za kike zilizotokana na mimea  (phytooetrogens).
KAZI YA DAWA HII.
1.dawa hii husaidia kubalance homoni za kike
( through NEGATIVE FEEDBACK MECHANISM) na hivyo kufanya mtu kuwa na usawa katika homoni zake na kupelekea kuepukana na tatizo hili.
2. Husaidia kupunguza matatizo yatokanayo na kikomo cha hedhi
3. Humkinga mwanamke asipate kansa zitokanazo na kuzidi kwa homoni za kike kama vile;
      Kansa ya matiti
      kansa ya shingo ya kizazi
      kansa ya utumbo nk.

NOTED :Ikumbukwe kuwa kupata maumivu wakati wa hedhi ni tatizo na sio kawaida kama inavyosemekana hivyo tumia njia hizi ambazo zinaungwa mkono na shirika la afya duniani (WHO) na shirika la kansa duniani kwani hupunguza kwa kiasi kikubwa kansa zitokanazo na KUZIDI KWA HOMONI YA KIKE

Asante Kwa kuwa pamoja nami Rafiki naomba uendelee kutembelea page hii kila siku na wape taarifa ndugu na jamaa zako waje tujifunze pamoja pia kama utahitaji Ushauri au utakuwa na la kunishauri naomba uniandikie ujumbe kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA ZA AFYA TEMBELEA KATIKA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

Imeandikwa na Dr Naytham S Masoud
Email nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

TAFADHALI SHARE NA LIKE BLOG HII

SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA WAKATI

FAHAMU SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI /KUTOPATA HEDHI KATIKA MPANGILIO MAALUMU (AMENORRHEA)

Asaalam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu msomaji wa page hii, napenda kukushukuru kwa kuungana Nami katika page hii kuendelea kutoa elimu kwa wanawake na wasichana kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayosababisha kukosa hedhi iliyo salama, kutokana na maswali yenu ya kwanini mwanamke huwa anakosa hedhi ilhali Hana mimba??nimeona ni vyema kuelezea hili tatizo kwa undani ili muweze kutambua vizuri tatizo hili ambalo kitaalamu linajulikana kama AMENORRHOEA

AMENORRHEA NI NINI??
hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi/kupitiliza siku za hedhi
~kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani
~kuna aina mbili za tatizo hili (amenorrhea)

(1)PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke/msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo Hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile KUOTA NYWELE SEHEMU ZA SIRI, KUOTA MATITI, NK ila bado hapati siku zake

(2)SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida Lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa

~NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio Sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa

~VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika Makundi makuu matatu ambayo ni vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo katika tezi ya pituitar, mfumo wa Uzazi na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke visababishi hivyo ni ÷
👉matatizo katika hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha ÷uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar, ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi,

👉uzito mdogo kuliko Kawaida

👉pituitar kushindwa kufanya Kaz vzur baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua

👉kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)
(proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo Hali ya kuwa proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi

👉kuwa na msongo wa mawazo ni hatari

👉kuziba kwa utando unaozunguka uke (HYMEN) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)

👉 Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri yani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari

👉ugonjwa wa kurithi wa GALACTOSEMIA unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya GALACTOSE katika damu

👉baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME

👉MENO PAUSE ~hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42_55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi hufanya haziwezi kufanya Kazi sawasawa

DALILI ZA TATIZO HILI
👉Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za ANDROGEN

👉kuongezeka uzito kupita kiasi

👉matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi

👉mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida

👉 uke kuwa mkavu

👉kutokwa jasho sana wakati  wa usiku

👉mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries

👉kutokupata hedhi katika mpangilio

MATIBABU
NA JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji pale patapobidi

NOTE :Ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiepusha na tatizo hili

👉ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI

👉TUMIA MAZIWA YA SOY /JUICE YA WATERMELON/MAJI YA MSHUBIRI

👉FANYA MASAJI KWENYE TUMBO LA CHINI KWA KUTUMIA MAJI YA UVUGUVUGU (UKIWA KTK BREED) HII ITASAIDIA KUONGEZA DAMU NYINGI KUTOKA

👉KULA CHAKULA  KISICHOTOKANA NA DAMU (VEGETARIAN DIET) CHENYE PROTIN NYINGI MFANO, NAZI, MAHARAGE, KOROSHO NA KARANGA
Hakikisha unazingatia haya ili kuepukana na madhara ya huu ugonjwa ambayo ni makubwa sana

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU
👉Mwanamke kuchelewa kuingia menopause hali huu ni mbaya kwani husababisha SARATAN YA MATITI kwa kias kikubwa
👉mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu
👉husababisha matatzo ya kutopata usingizi
👉matiti husinyaa na kupata hedhi Bila mpangilio,

ndugu Rafiki msomaji Asante kwa kuwa Nami muda wote kutoa elimu hii kwa jamii kama una MAONI/ USHAUR NIANDIKIE UJUMBE KUPITIA NAMBA NA EMAIL YANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA ZA AFYA TEMBELEA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLEASE USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA KUWAALIKA WENZAKO KATIKA PAGE HII NI VIZURI ZAIDI UKISHARE NA WENZAKO WAPATE ELIMU HII

TATIZO LA UVIMBE KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE (UTERINE FIBROID/LEIO MYOMAS)

FAHAMU UVIMBE KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE (UTERINE FIBROIDS/LEIO MYOMAS)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatull
Natumaini mnaendelea vizuri, leo tena napenda kuzungumzia tatizo la uvimbe katika kizazi tatizo(UTERINE FIBROIDS/LEIO MYOMAS) ambalo ni common  kwa wanawake wengi

FIBROIDS NI NINI??
~Ni Aina ya vivimbe vinavyoota kwenye misuli Laini ya mfuko wa uzazi
~tatizo hili huwakumba wanawake wengi ambapo huwapata kwa 5% wanawake wenye umri wa miaka 20_30 na 20% kwa wanawake wenye umri wa miaka 30_40 na zaidi ya 40% ni kwa wale wenye umri zaidi ya 40 hivyo kwa ujumla tatizo la fibroids huwapata wanawake wengi hasa katika umri wa kuzaa (reproductive age) hii inamaana kuwa kadri umri unavyokuwa mkubwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata uvimbe.
~tafiti zinaonyesha kuwa tatizo hili huwapata zaidi wanawake wa kiafrika kuliko wazungu pia huwapata zaidi wanawake ambao hawajazaa kabisa au wale ambao wamekaa Muda mrefu Bila kuzaa, pia wanawake wanene, na wale waliopata hedhi mapema wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu

AINA KUU ZA FIBROIDS
~(1)SUBMUSOCAL FIBROIDS ~hii hutokea ndani ya kizazi
~(2)INTRAMURAL FIBROIDS ~hii hutokea ndani ya nyama ya kizazi
~(3)SUBSEROL FIBROIDS ~hii hutokea nnje kwenye ukuta wa kizazi
~uvimbe huwa na ukubwa tofauti kwani huanza mdogo na baadae kuwa mkubwa sana na hata wakati mwingine mwanamke huweza kuonekana mjamzito, kwani uvimbe huu huweza kuwa mmoja mkubwa na wakati mwingine huwa zaidi ya mmoja na kutanda katika mfuko wa kizazi
~watu wengi wamekuwa wakihisi fibroids kitu ambacho sio kweli kwasababu fibroids sio kansa Bali ni uvimbe wa kawaida ambao hukua kwa kutegemea kichocheo au hormone ya OESTROGEN na ndio maana wakati wa kupata tatizo hili huwa ni kipindi cha kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi

CHANZO CHA TATIZO
~Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi ila Kuna sababu ambazo huweza kusababisha mwanamke kupata fibroids, sababu ambayo ni common kusababisha tatizo hili ni WINGI WA HOMONI YA OESTROGEN ambayo ipo katika mwili wa mwanamke na ndiyo hufanya Kazi  ya kusababisha mwanamke kupata hedhi pia mara nyingi uvimbe huu hukua mkubwa sana kipindi cha UJAUZITO kwasababu vichocheo vya OESTROGEN huongezeka na kuwa vingi ili kulinda makuzi ya mtoto pia ni mara chache watu walio kikomo cha hedhi kupata fibroids na wakipata Kuna hatari ya kuwa kansa
DALILI ZA FIBROIDS
~dalili za uvimbe katika kizazi cha mwanamke hushindwa kuonekana iwapo uvimbe ni mdogo na pia dalili hutegemea sehemu ilipo kwenye mfuko wa kizazi pia na ukubwa wake, pamoja na hayo dalili zake mara nyingi ni zifuatazo ÷
👉KUTOKWA NA DAMU YENYE MABONGE MABONGE KWA MUDA MREFU
👉KUTOKWA DAMU KATIKATI YA MWEZI NA HEDHI KUTOKUWA NA MPANGILIO
👉KUPATA MAUMIVU YA KIUNO HASA WAKATI WA HEDHI
👉KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA
👉KUPATA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO
👉KUKOJOA MARA KWA MARA
👉MIMBA KUHARIBIKA MARA KWA MARA
👉KUPUNGUKIWA NA DAMU MARA NYINGI
👉MIGUU KUVIMBA
👉MKOJO KUBAKI KWENYE KIBOFU
👉HAJA KUBWA KUWA NGUMU
👉UGUMBA

MATIBABU &  VIPIMO
~matibabu ya fibroids hufanyika kwa daktari kumkagua mgonjwa kwa kutumia mikono miwili au kupima (Bimanual examination) pia anaweza kutumia kipimo cha ULTRA SOUND ya nyonga kwani ni rahis kugundua uvimbe au kipimo cha MRI,
~matibabu huweza kulenga ya kutibu dalili au kupunguza uvimbe na pia iwapo mwanamke ana tatizo hili na hamna dalili zozote basi anaweza kufuatilia tu uvimbe Bila kutumia dawa kwasababu mwanamke anapofikia menopause (kukoma hedhi)  tatizo hili hutokewa
~wanawake wengi wana fibroids ndogo ndogo ambazo hazina dalili hivyo hushindwa kutambua mpaka pale wanapobeba ujauzito au kupima ndio hugundulika
~NJIA ZA KUTIBU UVIMBE MKUBWA
~(1)DAWA
~hapa mgonjwa hupewa matibabu ya dawa ambazo hurekebisha kiwango cha homoni ya OESTROGEN mfano wa dawa hizo ni DANAZOL,na Aina ya pili ni vidonge vya kutuliza maumivu ya fibroids
~(2)UPASUAJI
Upasuaji hufanyika kwa kutegemea na ukubwa wa uvimbe na wingi wa fibroids ambapo upasuaj huo ni wa Aina mbili
(A) MYCOMECTOMY ~hii ni njia ya Upasuaji hutumika kwa mgonjwa mwenye uvimbe mmoja mkubwa ulio katika sehem nzuri na Upasuaji huu ni kutoa uvimbe tu na kuacha kizazi hata hvyo Upasuaji wa njia hii uvimbe una nafasi kubwa ya kurudi
(B) TOTAL ABDOMINAL HYSTERECTOMY ~hii ni njia ya Upasuaji ambapo kizazi hutolewa na hufanyika ikiwa kizazi kina uvimbe mmoja mkubwa sana au vivimbe vikiwa vingi vingi

MADHARA MAKUBWA YA FIBROIDS
~Husababisha mimba kutoka mara kwa mara na hatimaye mtu kuwa mgumba, pia huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi
NOTED :ndugu rafiki hakikisha unaenda kupima Afya yako kila mwezi ili kujua maendeleo ya Afya yako kwani wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili la fibroids
IKIWA UNA MAONI/MASWALI/MAPENDEKEZO YOYOTE NIANDIKIE KUPITIA E-MAIL NA NAMBA YANGU HAPO CHINI

PIA KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham email:nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095
PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENTI, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

Jumapili, 9 Oktoba 2016

JE, WAZIJUA FAIDA ZA TANGAWIZI NA ASALI? SOMA HAPA ILI KUFAHAMU

FAHAMU FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI ;
Asaalam alaykum warhmatullah wabarakatul mpenzi msomaji wa page hii, ni matumaini yangu umzima kabisa,kumradhi Kwa ukimya wangu nilibanana na majukum ya hapa na pale ila sasa namshukuru ALLAH wepesi umepatikana na nimeweza kurejea tena hapa,
Leo napenda tufaham faida za tangawizi mwilini ambazo ni ...

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana,

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi,

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi,

4. Huondoa uvimbe mwilini,

5. Huondoa msongamano mapafuni,

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake,

7. Huondoa maumivu ya koo,

8. Huua virusi wa homa,

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini,

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills),

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo,

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi,

18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi,

19. Huongeza msukumo wa damu,

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo,

21. Huzuia damu kuganda,

22. Hushusha kolesto,

23. Husafisha damu,

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa,

25. Hutibu shinikizo la juu la damu,

26. Husafisha utumbo mpana,

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma,

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI,

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu,

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu,

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa,

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula,

34. Husaidia kuzuia kuharisha,

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu,

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa,

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi,

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito,

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis),

41. Huimarisha afya ya figo,

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha,

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita,

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha,

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium,

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene,

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mkojo hupita

Asante Kwa kuwa nami rafiki naomba usikose kushare na wengine ili waweze kutambua faida hizi pia kama unasumbuliwa na tatizo lolote lihusuyo afya usikose kuwasiliana nami ili kuweza kupata Ushauri zaidi

PIA KUSOMA MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

 Makala hii imeandikwa na Dr Naytham S Masoud
Email -nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

TAFADHALI SHARE NA WENGINE UJUMBE HUU WAPATE KUJIFUNZA

FAHAMU FAIDA 11 ZA KUNYWA MAJI YENYE NDIMU ASUBUHI



HIZI NDIO FAIDA 11 ZA KUNYWA MAJI YA NDIMU ASUBUHI 

 Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Nina imani mmeamka salama na mnaendelea vyema wapendwa ni jambo la kumshukuru mungu Kwa hakika 

Mpenzi msomaji nina imani umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).

Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.

Faida 1: Huchochea Mmeng’enyo Wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida 2: Huboresha Kinga Za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 Faida 3: Husaidia Unyonywaji Wa Madini Mwilini

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida 4: Husaidia Kinga Dhidi Ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida 5: Husaidia Kupunguza Hatari Ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

Soma pia: Madhara ya kula chumvi nyingi kwa afya ya binadamu

Faida 6: Usafishaji Wa Mwili Na Damu

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

 Faida 7: Kurekebisha Sukari Katika Mwili


Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

Faida 8: Dawa Ya Kikohozi Na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

Faida 9: Inasaidia Urekebishaji Wa Ngozi Na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.

Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

 Faida 10: Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

 Faida 11: Kuondoa Harufu Ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

 Anza Siku Kwa Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Siku,
Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.
 NB :HAIFAI KWA WENYE VIDONDA VYA TUMBO 
  
 Asante Kwa kuwa nami kupata elimu hii mpenzi msomaji kama una swali au maoni unaweza kuniandikia ujumbe kupitia namba na emails yangu hapo chini 

Kwa makala zaidi za afya naomba utembelee blog yangu ya 
Naythamhealthcare.blogspot.com 

makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud 
email nsalum9998@gmail.com
0689538628

  
TAFADHALI SHARE NA WENGINE WAPATE KUJIFUNZA ELIMU HII