BREAKING
BannerFans.com

Alhamisi, 17 Novemba 2016

TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS)

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS) LINAVYOWAANGAMIZA NA KUWAKOSESHA RAHA WANAWAKE

Asalam alaykum warhmatullah wabarakatul mpenzi msomaji wa makala hii natumaini unaendelea vizuri na majukumu ya kila siku, namshukuru Mungu kuniwezesha leo tena kuandika makala ili kukuwezesha ndugu msomaji kufahamu mambo mengi kuhusu Afya ya mwanamke na mzunguko mzuri wa hedhi, leo napenda kuzungumzia tatizo la kuvimba kwa kizazi cha mwanamke ambapo kitaalamu tunasema ni ADENOMYOSIS pia tatizo hili kwa zamani lilijulikana kama ENDOMETRIOSIS INTERNA

ADENOMYOSIS NI NINI?
~Ni tatizo ambalo nyama hutokea na kukua kama tabaka au ukuta mwingine juu ya misuli ya kizazi(ectopic glandular tissues)
~tatizo hili huwaathiri zaidi wanawake walio kati ya miaka 35_50, ingawa katika Hali isiyo ya kawaida hutokea katika umri wa chini ya miaka 35
~tatizo hili la kuvimba kwa kizazi linapotokea huambatana na damu nyingi wakati wa hedhi na kupata maumivu makali wakati wa hedhi pia maumivu huongezeka zaidi pale tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi na hivyo mwanamke mwenye tatizo hili la kuvimba kwa kizazi hupata maumivu makali chini ya tumbo ktk kitovu Muda wote pasipo kupata damu ya hedhi hata kama tarehe za kupata damu (period) zimefikia, pia damu huweza kutoka kwa wingi pia kizazi huendelea kuvimba kutokana na tabaka la ndani (basal endometrium) kujipenyeza ndani ya misuli ya kizazi na hivyo kusababisha kila siku kizazi kuendelea kukua na mwanamke kuonekana kama ana ujauzito na tumbo huwa gumu hata hivyo tatizo hili ni tofauti na tatizo la uvimbe katika kizazi (fibroids)

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUVIMBA KWA KIZAZI
~Chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijafanikiwa kuwa wazi ingawa misuli ya kizazi (uterine trauma) huchangia hili kwa kuwa huondoa ukingo wa tabaka la ndani ya kizazi kuelekea katika misuli ya kizazi pia utoaji wa mimba hovyo husababisha mirija kuchubuka pia matokeo mabaya ya uwekaji wa lupu

DALILI ZA TATIZO HILI
Dalili au viashiria vya tatizo hili ni vingi ila hata hivyo Kuna baadhi ya wanawake wenye tatizo hili hawaonyeshi dalili yoyote huku kizazi kikizid kuvimba na wengine huhisi maumivu makali ya kizazi Muda wote au wakati wa hedhi
Dalili zenyewe ni Hizi
👉chembechembe za tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi huendelea kutoa damu hivyo kusababisha damu kuvujia ndani kwa ndani Bila damu hiyo kutoka nnje
👉mwanamke huhisi uchungu wa uzazi na kuhisi kama vile anataka kujifungua kwa kuwa hupata shinikizo ukeni
👉mwanamke huhisi maumivu makali chini ya tumbo Muda wote na kila akienda katika hospital hukutwa ana uti kitu ambacho sio kweli
👉mwanamke huhisi maumivu makali zaidi kipindi cha upevushaji mayai (ovulation) au kipindi cha period (hedhi)
👉mwanamke huhisi mkojo kila wakati kutokana na kibofu kugandamizwa na shinikizo la kizazi
👉mwanamke hutoka damu kupita kiasi hadi pedi huwa hazitoshelezi pia wakati wa hedhi tumbo hubana au kukaza (abdominal eramps) Muda wote na mwanamke hutamani kuinama tu

MATIBABU NA VIPIMO
matibabu ya tatizo hili hufanyika katika kliniki Za akina mama kwenye hospital za mkoa, private na daktar hutibu kutokana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo vya MRI, ULTRASOUND na matibabu hayo huweza kuwa ya dawa za HOMONI kutegemea na ukubwa wa tatizo pia tiba nyingine ni upasuaji hasa wa kuondoa kizazi kitu ambacho hugharim sana maisha ya mahusiano iwapo mhusika hakuzaa na pia endapo mwanamke atapata tatizo hili akiwa mjamzito basi mimba Yake hutoka na hupata uchungu mapema kabla ya siku ya kujifungua

USHAURI :WANAWAKE WENGI HUWA NA DESTURI YA KUPUUZA KWENDA HOSPTAL KWA KUONA TATIZO NI DOGO HVYO NDUGU RAFIKI HAKIKISHA UNAENDA KUPIMA AFYA YAKO MARA KWA MARA ILI KUWEZA KUTAMBUA MATATIZO MAPEMA HIVYO TUACHE TABIA YA KUPUUZIA KITU HATA KAMA NI KIDOGO
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia email na namba yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA ZA AFYA TEMBELEA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email:nsalum998@gmail.com/+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

Hakuna maoni :