FAHAM UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu zangu ni matumaini yangu mnaendelea vyema kabisa,napenda kuwataka radhi na kuwapa pole Kwa ukimya wangu kutokana na kupisha shughuli za uchaguzi, Nimepokea emails zenu nyingi sana za kunimiss nimefarijika napenda kuwaambia nami NIMEWAMISS NA NINAWAPENDA WOTE pamoja na hayo nimeona emails zenu zinazohusu magonjwa mbalimbali yanayowasumbua wanawake wengi na hivyo Leo hii napenda nianze na ugonjwa wa PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI )
UGONJWA WA PID NI NINI??
~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)
VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID
~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa PID zipo njia kadhaa hatarishi kusababisha maambukizi haya Nazo ni ÷
👉kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi(IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
👉Kufanya ngono isiyo salama
👉Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika
👉Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID
👉Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama
DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni
👉Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
👉Kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
👉Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
👉Kutokwa na hedhi bila mpangilio
👉kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya
VIPIMO NA MATIBABU YA UGONJWA WA PID
Matibabu ya tatizo hili yanapatikana kote nchini kwa kufata misingi ya utabibu kuzingatia majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali ili kuweza kubaini tatizo kwa kufanya vipimo tofauti
MFANO
👉FULL BLOOD PICTURE _kipimo hiki kinatumika ili kuweza kutambua aina mbalimbali za chembe damu zilizoathiriwa na maambukizi ya PID
👉CERVICAL CULTURE_Hutumika ili kujulia aina ya vimelea waliosababisha PID
👉ULTRASOUND _hutumika kuangalia katika nyonga kama kuna athari yoyote imetokea katika mfumo wa uzazi
~mara baada ya kufanya vipimo na mgonjwa kugundulika kama ameathirika na tatizo hili mara nyingi dawa za antibiotics ambazo ni DOXYCYCLINE,CEFOXITIN,MYCIN,GENTAMYCIN,CLINDAMYCIN,SULBACTAM,AMPICILLIN, huhusika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa huu lakini ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali ambayo imewekwa na mamlaka na wizara ya afya kati ya sehem moja hadi nyingine hivyo si ruhusa kujinunulia dawa na kumeza pasipo ushauri wa daktari
NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉JIWEKEE TABIA YA KUFANYA VIPIMO MARA KWA MARA HASA KIZAZI
👉USIFANYE MAPENZI MARA BAADA YA KUJIFUNGUA AU MIMBA KUTOKA MPAKA UTAKAPOHAKIKISHA SHINGO YA UZAZI IMEFUNGA VEMA
👉KUWAHI KUONANA NA DAKTARI UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA
👉KUWA MSAFI NA KULA LISHE BORA
NOTED:NDUGU RAFIKI UONAPO DALILI ZA UGONJWA HUU WAHI KUPATA MATIBABU KWANI UGONJWA HUU NI MKUBWA HUWEZA KUSABABISHA UGUMBA IKIWA HAUTAPATA TIBA VIZURI
Kwa makala zaidi za afya tembelea blog yangu hapo chini
naythamhealthcare.blogspot.com
asante kwa kuwa nami kusoma ujumbe huu rafiki kama una MAONI/MASWALI NIANDIKIE KUPITIA NAMBA NA EMAIL YANGU HAPO CHINI PIA TAFADHALI NISAIDIE KUIFIKISHA ELIMU HII KWA WENGINE
Makala hii imeandaliwa na
Dr Naytham
+255623026602/+255746465095
email;nsalum998@gmail.com
naythamhealthcare.blogspot.com
USISAHAU KULIKE,KUKOMENT NA KUSHARE NA RAFIKI ZAKO

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni