BREAKING
  • FANGASI UKENI

    Pata suluhisho la tatizo la fangasi ukeni pamoja na ushauri utakaokufanya uwe salama daima

  • TIBA YA NGUVU ZA KIUME

    Okoa nyumba yako kwa kupata dawa itakayo ongeza nguvu zako za kiume na kudumisha unyumba daima

  • SULUHISHO LA U.T.I

    Je hauna ufahamu wowote kuhusu U.T.I ?Je Unakabiliwa na tatizo la U.T.I?Wasiliana nami nikujuze zaidi huenda una tatizo la U.T.I lakini haujijui,na kama unalo basi tiba yake ipo

  • TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

    Je Umesumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu pasina kupata suluhisho,wasiliana nami nikupatie dawa itakayoondoa tatizo lako kabisa

BannerFans.com

Jumamosi, 7 Januari 2017

TIBA SAHIHI YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

FAHAMU TIBA YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu mpenzi msomaji  katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote,
 Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa na  Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake,
 
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuna sababu zaidi ya 250 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume,Mtu anaweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo

MAANA YA NGUVU ZA KIUME
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.

Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za  acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi;

2. Uume kusimama kwa uregevu;

3. Kuwahi kufika kileleni;

4. Kuchelewa sana kufika kileleni ( kushindwa kufika kileleni kabisa);

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa;

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo;

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji;

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Mpendwa  msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.

Lakini nini kinachopelekea viungo hivyo vishindwe kufanya kazi vizuri?
Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia).

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua TAHADHARI kabla ya HATARI!

KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI!
Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana!

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo. Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanaume  wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana.

Nani anaweza kutibu nguvu za kiume?
Kuna watu wengi sana hivi leo wanaodai kutibu nguvu za kiume. Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kweli! Ni watu wachache sana wana uwezo wa kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Utakuta mtu anatangaza dawa ya aina moja kuwatibu watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume. Tabia hii pia imejengeka kwa baadhi ya watu, hupiga simu na kuuliza moja kwa moja, "Daktari, dawa za nguvu za kiume ni shilingi ngapi?"

 Kila mwanamume ana sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume. Kama wanaume 100 waliopungukiwa nguvu za kiume watajipanga mstari, kila mmoja atakuwa na sababu yake na chanzo chake cha kupungukiwa nguvu za kiume tofauti kabisa na mwingine.

Hii humaanisha kila mgonjwa atakuwa na dawa yake ya kipekee kabisa tofauti na mwingine. Sasa itashangaza kuona huyu kapungukiwa nguvu za kiume kutokana na mishipa ya ateri kutofanya kazi vizuri, na yule kapungukiwa nguvu kutokana na kuvimba kwa tezidume,Halafu wote wapate dawa aina moja! Hiki ndicho kinachofanyika na watu wengi wamepoteza pesa na muda kwa matibabu yasiyokuwa na maana.

Yahitajika daktari mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo, ndiye anayeweza kutibu tatizo la nguvu za kiume. Yaani, daktari ambaye anajua vizuri ndani na nje utendaji wa figo, ini, moyo n.k; awe ni daktari wa tiba asilia au daktari wa tibakemikali (yaani daktari wa hospitali) siyo kila mtu tu au kila daktari. Hata kama utakwenda kwenye hospitali kubwa yoyote duniani unayoijua, na ukagonga hodi katika chumba cha daktari, ukamwambia, "Nina tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume," atakurifaa kwa daktari maalumu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo. Hata kwa madaktari wa tiba asilia, hali ni hivyo hivyo, lazima ukutane na ambaye amebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Kwa sababu unapotibu nguvu za kiume unakuwa unatibu viungo vya mwili kwa ujumla. Daktari aliye mtaalamu anakuwa ana uwezo wa kutambua tatizo la kiungo kilichokorofisha mwilini kutokana na kumhoji mgonjwa; na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiridhisha kwa vipimo.

LISHE MUHIMU KUREJESHA NGUVU ZA KIUME
wakati mwingine mwanamme hupatwa na tatzo la Nguvu Za Kiume kutokana na kukosa madini lishe muhimu yanayohitajika mwilini mwake
Naam tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.

Antioxidant Nutrients

Upungufu wa vitamin E, vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa (sperm motility). Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa (International Units - IU) 100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza kumzalisha mwanamke (infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba mwanamke. Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye shahawa (sperm count) na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Tafiti pia zimeonyesha kwamba selenium husaidia uogeleaji wa shahawa.

Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA) ya vitamin C ni miligramu 90. Mwanaume anayevuta sigara anahitaji miligramu 125. Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits), cantaloupe, kiwi, maembe, strawberries, broccoli, cauliflower, pilipili nyekundu na juisi ya nyanya. Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source) na 22 (synthetic). Vyakula muhimu ni pamoja na ngano, karanga na jamii zake, mafuta ya mimea, mbegu zisizokobolewa (whole grains). Selenium RDA ni 15 micrograms. Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood, kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga, vitunguu swaumu.

Vitamin B12

Upungufu wa vitamin B12 hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility. Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa zake, mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).

Zinc

Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa. Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc. Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi kidogo cha homoni za kiume (low testosterone levels). Wanaume wenye shida hiyo wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba. RDA ya zinc ni miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8). Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza, dark turkey meat, lentils, ricotta cheese, tofu, yogurt, spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya. Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.

L-carnitine

Husaidia kuongeza sperm count. Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye nyama na maziwa

NOTED;KABLA YA MATUMIZI YA DAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NI VYEMA UKAWASILIANA NA DAKTARI WAKO WA KARIBU ILI KUPATA USHAURI ZAIDI

Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUNZA

Jumamosi, 19 Novemba 2016

UGONJWA WA KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA/BAWASIRI (HEMORRHOIDS)

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA (HEMORRHOID) NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, sifa njema anastahiki Allah Subuhhanah'wataala Kwa afya na uzima alotujaalia,
Leo tena napenda kuzungumzia ugonjwa wa Bawasiri/hemorrhoids)
Naam watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba idadi yake inazidi kuongezeka

BAWASIRI/HEMORRHOIDS
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI
~Kuna Aina mbili za bawasiri
(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI ~hii  hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia

(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe

(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi

(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

CHANZO CHA TATIZO
~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO VIZURI
👉MATATIZO YA UMRI
👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
👉UZITO KUPITA KIASI
👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

DALILI ZA BAWASIRI
dalili za ugonjwa wa Bawasiri ni :

👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana

VIPIMO NA UCHUNGUZI
Vifuatavyo ni vipimo vinavyotumika kugundua ugonjwa wa Bawasiri
Digital rectal examination
Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

MATIBABU

Matibabu ya mwanzo ya ugonjwa huu  kawaida huwa ni ongezeko la kula chakula kilicho na faiba(high fibre) na  vinywaji Kwa wingi ili kudumisha haidresheni pia  dawa za kutibu maambukizi  husaidia kwa maumivu na mapumziko
Lakini pia kuna  Baadhi ya taratibu kubwa zinaweza kutekelezwa ikiwa dalili ni kali au hazistawi kwa mwelekeo wa matibabu ya awali
Mfano wa taratibu hizo ni :
(1)Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.

(2)Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
Coagulation (infrared, laser and bipolar)

(3)TCM MEDICAL-hapa Mgonjwa hushauriwa kutumia Dawa Aina ya TCM  kulingana na ukubwa wa tatizo Lake ambazo husaidia kurahisisha mfumo wa mmeng'enyo na kuponya chanzo cha tatizo
Mfano wa Dawa hizo ni
(1)MEAL CELLULOSE TABLET 700MG
/MEAL CELLULOSE OR DIETARY FIBER. Meal cellulose,also referred to dietary fiber,includes all parts of plant foods that the body can not digest or absorb. Therefore, it passes relatively intact through our stomach,small intestine,colon and out of our body.


(2)SPIRULINA PLUS CAPSULE 500MG
is a  natural “algae” (cyanbacteria) powder that is incredibly high in protein and a good source of antioxidants, B-vitamins and other nutrients. When harvested correctly from non-contaminated ponds and bodies of water, it is one of the most potent nutrient sources available



(3)PARASHIELD CAPSULES 500MG
(4)ALOE VERA PLUS CAPSULE 500MG

Upasuaji;
         Hemorrhoidectomy
         Stapled hemorrhoidopexy
Ni hatua ya mwisho iliyotengwa Kwa wale wanaokosa mabadiliko ingawaje sio nzuri kiafya Kwa ujumla

NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI

badilisha mfumo wako wa chakula,
Kula High fibre diet(vyakula vyenye nyuzinyuzi  kama mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.

Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)

Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa

Fanya mazoezi mepesi na sio mazoezi magumu

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI ugonjwa wa Bawasiri usipotibiwa huleta athari zifuatazo Kwa Mgonjwa
👉kupata upungufu wa damu (anemia)
👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake kwasababu husababisha maumivu Kwa Mwanamke wakati wa tendo la ndoa
👉kuathirika kisaikolojia
👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali

NOTED:
NDUGU RAFIKI KAMA UNA UGONJWA HUU EPUKA KULA NYAMA NYEKUNDU NA PILIPILI PIA UNAWEZA  WASILIANA NAMI KWA USHAURI WA MATIBABU YA KUONDOA TATIZO HILI PASIPO KUFANYA UPASUAJI
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUNZA

Alhamisi, 17 Novemba 2016

SABABU ZA UKE KUTOA HARUFU MBAYA

FAHAMU SABABU ZA MWANAMKE KUTOA HARUFU MBAYA UKENI

Asalam alaykum warhmatullah wabarakatull
Ni matumaini nyote mnaendelea vyema, nami alhamdulillah ala kul Hali naendelea vyema
 Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu na ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni,leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK,
~kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo
~majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria
~Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa hayawashi na huwa na rangi nyeupe au njano pia huwa na asidi ya LACTIN ambayo huzuia bacteria kuzaliana
~mwanamke hutoa kiasi cha grams 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa kizazi na grams 3 za ute mwepesi kila siku, kiwango hicho kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi pia Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika na Kuna wakati pia huwa mzito wa rangi ya njano hautoi harufu

VISABABISHI VYA TATIZO HILI
~sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili

(1)BACTERIA VAGINOSIS
~Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili

(2)TRICHOMONAS
~maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili

(3)YEAST INFECTION
~kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina)
~maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa na tendo la ndoa, mambo ambayo huchangia tatizo hili ni MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA, MAWAZO, UJAUZITO, KISUKARI NA MATUMIZI YA ANTIBIOTICS

(4)VAGINAL OR CERVICAL CANCER,
~mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba

(5)SEXUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs)~Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili
(6)POOR HYGIENE ~tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo

DALILI ZA TATIZO HILI
~kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake
@UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU
~huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga
@UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA
~Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo
@UCHAFU MWEUPE MZITO KAMA JIBINI
~mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
@UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI
~uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke

~MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE
~Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo
👉EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
👉EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
👉PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
👉TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
👉SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA KUZIPIGA PASI
👉KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
👉EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
👉EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI,
NOTED :wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo  kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatkan kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha hivyo ni heri ukaacha kutumia kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana


Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAJIFUNZE

UGONJWA WA FANGAS UKENI (VAGINAL CANDIDIASIS)

FAHAM NAMNA YA KUJITIBU NA KUJILINDA DHIDI YA UGONJWA WA FANGASI UKENI (VAGINAL CANDIDIASIS)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu msomaji wa page hii,kutokana na kupokea maoni na maswali yenu leo nimependa kuzungumzia ugonjwa wa fangasi ukeni ambao ni common hususani kwa wanawake,

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua ni tatizo kubwa sana Duniani 75%ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili,na maambukizi haya ya fangasi  husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS lakini pia maambukizi haya hujulikana kama YEAST INFECTIONS /THRUSH

CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke
bacteria Hawa huishi katika sehemu hizo Bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, MFANO mabadiliko katika Hali ya PH
tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0_4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile MATUMIZI YA MADAWA YA ANTIBIOTICS eg AMPICILLINE, CIPROFLAXINE, AMOXYLINE, DOXYCYCLINE, ERTHROMYCINE, NK pia kupungua kwa Kinga kutokana na magonjwa mbalmbal nk

maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu KUU mbili nazo ni ÷
(1)MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
~katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi Mara moja hadi nne kwa mwaka pia Dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS

(2)MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi Zaidi ya Mara nne au Zaidi kwa mwaka pia Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha UJAUZITO, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk

VIHATARISHI VYA MAAMBUKIZI YA FANGASI KATIKA UKE
~Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambazo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri
~magonjwa ya saratani ya tezi koo la Chakula (thyroid cancer)
~wanawake wenye umri wa miaka 20_30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira na vitu wanavyotumia
~upungufu wa Kinga mwilin kutokana na magonjwa hatar ya saratani, kisukari, ugonjwa wa mononucleosis nk
~matumizi ya vidonge vya majira
~msongo wa mawazo
~kujamiana kwa njia ya kawaida Mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex)
~matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia
~kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy)
~ujauzto (husababisha kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini
~kuwa na utapiamlo (malnutrition
~kuvaa nguo za ndani ziszo kauka vzur
~kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehem za siri

DALILI ZA UGONJWA WA FANGASI UKENI
👉kuwashwa sehem za siri
👉kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana (superficial dysapareunia)
👉kuhisi kuwaka moto sehemu za siri Mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation
👉kupata vidonda ukeni (soreness
👉kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nnje wa uke (labia minora
👉kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa MWEPESI au MZITO au majimaji
NOTED :Dalili na viashiria hivi huwa mbaya Zaidi mwanamke anapokua mwezini

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA FANGASI UKENI
Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals).  Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi
Cotrimazole na fluconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara lakini pia pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia kwakuwa Dawa zetu hizi zimekua zikitibu dalili na si chanzo cha tatizo hivyo ni muhimu kupata tiba mbadala na Ushauri zaidi  unapoona inajirudia

 pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kujikinga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kufanya mambo yatakayotusaidia kutopata ugonjwa huu kwa kuzingatia kanuni ya afya na USAFI
👉Vaa chupi ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka kutumia chupi aina ya synthetic underwear
👉epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya hivyo ni vyema wapenzi wote wawili mkapata matibabu ya fangasi na mjitahidi kuwa waaminifu
👉kula mlo wenye virutubsho muhimu
👉epuka kuoga maji ya moto sana (Hot baths) tumia maji ya uvuguvugu
👉osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa Safi
👉epuka mavazi yote ya kubana ukeni
👉tumia ped na pantiliner zenye anions zenye uwezo wa kufyonza haraka (NEPLILY)
👉kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni
👉epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni
👉 epuka kutumia sabuni za kemikali

FAHAMU PEDI BORA ZA NEPLILY
ped za neplily zimetengenezwa kwa technologia ya hali ya juu,neplily pads na pantliner zimetengenezwa kwa anion chip technology,
Anion ni negative particles ambazo zinatoa oxygen pale zinapogusana na mwili wako,
Joto la mwili linapokutana na pedi au pantliner inaachia negative particles ambazo mwisho wa siku inatoa hewa safi ya oxygen.
anions hizi zinapatikana kwenye maporomoko ya maji,chemichemi ya maji kwenye misitu,mvua za acidi,moshi wa misitu baada ya kuunguzwa n.k.
faida za anion chip

1.inauwezo wa kuondoa muwasho,bacteria,fungus wa aina yoyote kipindi cha hedhi
2.inaondoa harufu mbaya
3.inarekebisha mzunguko na kuweka homoni sawa.
4.inapunguza uwezekano wa kupata ugumba
5.inaondoa msongo wa mawazo na uchovu kipindi cha Hedhi
6.inarekebisha mfumo wa homoni za mwili
7.pantliners pia zinatumika na wanaume wenye prostatic hypertrophy, bawa siri na kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa
8.inauwezo wa kuondoa uvimbe na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba.
9.inaimarisha kinga ya mwili na kujikinga na matatizo yote ya uzazi.
10.inaondoa matatizo yote ya uzazi hasa baada ya kuogelea kwenye mabwawa ya kuogelea.
10.inatibu uti.
kwa ujumla neplily pads na pantiliner zina uwezo mkubwa wa kutokomeza matatizo yote yanayowakumba wanawake wakiwa kwenye siku zao.kama kuumwa kichwa,msongo wa mawazo,kuchoka,kuumwa tumbo,kuwa na flow kubwa na mengine mengi
ZITUMIENI ZITAWASAIDIA

NOTED :NDUGU MSOMAJI KAMA UNA MAONI/USHAUR NA UNASUMBULIWA NA TATIZO HILI WASILIANA NAMI NIANDIKIE UJUMBE KUPITIA NAMBA NA EMAIL HAPO CHINI

Makala hii imeandikwa na Dr Naytham S Masoud
nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

KUPATA MAKALA ZAIDI ZA AFYA WAWEZA TEMBELEA BLOG HII naythamhealthcare.blogspot.com

naimain umejifunza Nami nashukuru kwa wew kujifunza hivyo nakuomba nawe uwafikishie elimu hii wengine KWA KUSHARE, KUKOMENT NA KUWAALIKA WENZAKO WALIKE PAGE HII

TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI (OVARIAN CYST)

FAHAMU ATHARI ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatull,
 Naam natumaini mnaendelea vizuri napenda kumshukuru Mungu kwa kunijaalia Afya kuweza kuandika makala hii inayohusu uvimbe katika mayai ya mwanamke hivyo ungana nami rafiki kupata elimu hii

OVARIAN CYST NI NINI??
~Ni uvimbe unaotokea katika mayai ya mwanamke (ovarian)
~uvimbe huo hutokana na mkusanyiko wa maji maji yanayozungukwa na kutu nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke
~uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa rika tofauti na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofika umri wa kushika ujauzito
~uvimbe huu huweza kuwa na ukubwa wa cm3_cm30 na unaweza kujaza tumbo lote

AINA ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE
(@)HEMORRHAGIC CYST ~hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa Aina yoyote ule ambao umeshajitengeza tayari,pia uvimbe huu huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu (kushoto /kulia)

(@)FOLLICULAR CYST ~hii ni Aina ya uvimbe unaotokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu una ukubwa wa wastani 2:3 kwa upana, uvimbe huu hauna dalili yoyote na hupotea yenyewe baada ya Muda

(@)CORPUS LUTEUM ~hii ni Aina ya uvimbe ambazo unatokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu husinyaa na kupotea wenyewe ingawa wakati mwingine huweza kujaa maji na kusababisha tumbo kuvimba upande mmoja

(@)DERMOID CYST ~uvimbe huu hujulikana kama MATURE CYST TERATOMA, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika ujauzito na uvimbe huu huweza kukua nchi 6 kwa upana na ndani Yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mifupa, mafuta na cartilage, pia uvimbe huu huweza kuwa mkubwa zaidi na kujizungusha hivyo huathiri mzunguko wa damu na hivyo kusababisha maumivu makali ya nyonga na tumbo.

(@)POLYCYSITIC APPEARING CYST ~huu ni uvimbe mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijiuvimbe vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye Afya njema na wale wenye tatizo la homorne

(@)CYSTEDENOMA ~hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea kwenye tissue za ovary na hujazwa na maji maji Aina ya kamasi pia uvimbe huu una ukubwa wa nch, 12 au zaidi kwa upana

(@)ENDOMETRIOSIS ~huu ni uvimbe unaosababishwa na uwepo wa Aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama ENDOMETRIUM kwenye mayai ya mwanamke, uvimbe huu huathiri wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu makali (sugu) ya nyonga (CHRONIC PELVIC PAIN) wakati wa hedhi, pia uvimbe huu una rangi nyekundu ya kahawia (reddish brown) na una ukubwa wa 0.75_8 inches


VIHATARISHI VYA TATIZO HILI
👉kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka (IRREGULAR MENSTRUATION CYCLE)
👉kuwa na mafuta mengi tumboni
👉kukosekana kwa uwiano wa vichocheo mwilini (hormone imbalance)
👉kuvunja ungo mapema yani kuanzia miaka 11kushuka chini
👉kutumia dawa za kemikali maana zina side effects

DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI
👉mwanamke kupata maumivu /kichomi ambayo huwa hayana Muda maalumu huchoma ukeni, kiunoni, mgongoni, mapaja, NK
👉kuhisi tumbo kuwa zito limejaa au kuvimba
👉kupata maumivu makali katika matiti
👉kutopata hedhi katika mpangilio
👉kuongezeka uzito mara kwa mara
👉kupata maumivu katika mbavu
👉kuumwa kichwa mara kwa mara
👉nywele kukua haraka kila wakati
👉kupata maumivu makali wakati wa hedhi
👉kuhisi kichefchef (kutapika)
👉kupata maumivu makali ya nyonga
👉kuhisi uchovu
Kila wakati
👉kutokwa na matone ya damu
👉kutoshika mimba
👉mabadiliko katika upatikanaji wa haja
@haja ndogo kutoka Bila kujielewa
(b) haja kubwa kuwa ngumu

VIPIMO NA MATIBABU
Matibabu hufanyika kwa kuangalia Majibu yaliyopatikana katika vipimo, Kuna vipimo vingi vya kuona tatizo hili kama vile ENDOVAGINAL ULTRA SOUND, COMPLETE BLOOD COULD, SERUM CA 125 ASSAY, URINE FOR PREGNANCY, baada ya daktar kupata Majibu ndio huangalia tiba inayoendana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya Aina mbili

(@)MATIBABU YA DAWA
~tiba hii huhusisha matumizi ya dawa za upangaji uzazi kwa Muda wa wiki 4_6, matumizi ya dawa Hizi kwa Muda mrefu huzuia kutokea tena uvimbe katika kizazi kwasababu dawa Hizi hufanya Kazi ya kuzuia mayai kutotoa mayai ya uzazi (ovums) pia dawa Hizi hazipunguzi uvimbe uvimbe kwasababu uvimbe utapotea wenyewe baada ya Muda

(B) TIBA YA UPASUAJI
~katika tiba hii ya upasuaji Kuna Aina mbili

(1)EXPLORATORY LAPARATOMY
~katika tiba hii mgonjwa hupasuliwa tumboni na daktar huweza kuondoa uvimbe, upasuaji huu hufanyika kwa mwanamke mwenye uvimbe ambao hauwezi kupotea na mkubwa kuanzia 5cm_10cm

(2)LAPARASCOPIC SURGERY
~huu ni upasuaji ambao daktari hupasua sehem ndogo na kutumbukiza mpira maalumu ambao una kamera kwa mbele na huondoa uvimbe katika mayai, upasuaji huu hupendwa na wanawake wengi kwasababu hauachi kovu lolote na mara nyingi hufanyika kwa uvimbe mmoja
NOTED :NDUGU RAFIKI hakikisha unaenda kupima Afya yako mara nyingi kwani Kuna watu wapo na tatizo hili ila wanashindwa kuelewa au hawajitambui hivyo ni bora ukaepuka ugonjwa huu kwani madhara Yake ni kusababisha UGUMBA.
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali, maoni, mapendekezo yoyote niandikie kupitia email  na namba yangu hapo chini

KUSOMA MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA KATIKA BLOG HII NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
email:nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095
PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS)

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA KIZAZI CHA MWANAMKE (ADENOMYOSIS) LINAVYOWAANGAMIZA NA KUWAKOSESHA RAHA WANAWAKE

Asalam alaykum warhmatullah wabarakatul mpenzi msomaji wa makala hii natumaini unaendelea vizuri na majukumu ya kila siku, namshukuru Mungu kuniwezesha leo tena kuandika makala ili kukuwezesha ndugu msomaji kufahamu mambo mengi kuhusu Afya ya mwanamke na mzunguko mzuri wa hedhi, leo napenda kuzungumzia tatizo la kuvimba kwa kizazi cha mwanamke ambapo kitaalamu tunasema ni ADENOMYOSIS pia tatizo hili kwa zamani lilijulikana kama ENDOMETRIOSIS INTERNA

ADENOMYOSIS NI NINI?
~Ni tatizo ambalo nyama hutokea na kukua kama tabaka au ukuta mwingine juu ya misuli ya kizazi(ectopic glandular tissues)
~tatizo hili huwaathiri zaidi wanawake walio kati ya miaka 35_50, ingawa katika Hali isiyo ya kawaida hutokea katika umri wa chini ya miaka 35
~tatizo hili la kuvimba kwa kizazi linapotokea huambatana na damu nyingi wakati wa hedhi na kupata maumivu makali wakati wa hedhi pia maumivu huongezeka zaidi pale tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi na hivyo mwanamke mwenye tatizo hili la kuvimba kwa kizazi hupata maumivu makali chini ya tumbo ktk kitovu Muda wote pasipo kupata damu ya hedhi hata kama tarehe za kupata damu (period) zimefikia, pia damu huweza kutoka kwa wingi pia kizazi huendelea kuvimba kutokana na tabaka la ndani (basal endometrium) kujipenyeza ndani ya misuli ya kizazi na hivyo kusababisha kila siku kizazi kuendelea kukua na mwanamke kuonekana kama ana ujauzito na tumbo huwa gumu hata hivyo tatizo hili ni tofauti na tatizo la uvimbe katika kizazi (fibroids)

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUVIMBA KWA KIZAZI
~Chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijafanikiwa kuwa wazi ingawa misuli ya kizazi (uterine trauma) huchangia hili kwa kuwa huondoa ukingo wa tabaka la ndani ya kizazi kuelekea katika misuli ya kizazi pia utoaji wa mimba hovyo husababisha mirija kuchubuka pia matokeo mabaya ya uwekaji wa lupu

DALILI ZA TATIZO HILI
Dalili au viashiria vya tatizo hili ni vingi ila hata hivyo Kuna baadhi ya wanawake wenye tatizo hili hawaonyeshi dalili yoyote huku kizazi kikizid kuvimba na wengine huhisi maumivu makali ya kizazi Muda wote au wakati wa hedhi
Dalili zenyewe ni Hizi
👉chembechembe za tabaka la ndani ya kizazi linapojikita katikati ya misuli ya kizazi huendelea kutoa damu hivyo kusababisha damu kuvujia ndani kwa ndani Bila damu hiyo kutoka nnje
👉mwanamke huhisi uchungu wa uzazi na kuhisi kama vile anataka kujifungua kwa kuwa hupata shinikizo ukeni
👉mwanamke huhisi maumivu makali chini ya tumbo Muda wote na kila akienda katika hospital hukutwa ana uti kitu ambacho sio kweli
👉mwanamke huhisi maumivu makali zaidi kipindi cha upevushaji mayai (ovulation) au kipindi cha period (hedhi)
👉mwanamke huhisi mkojo kila wakati kutokana na kibofu kugandamizwa na shinikizo la kizazi
👉mwanamke hutoka damu kupita kiasi hadi pedi huwa hazitoshelezi pia wakati wa hedhi tumbo hubana au kukaza (abdominal eramps) Muda wote na mwanamke hutamani kuinama tu

MATIBABU NA VIPIMO
matibabu ya tatizo hili hufanyika katika kliniki Za akina mama kwenye hospital za mkoa, private na daktar hutibu kutokana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo vya MRI, ULTRASOUND na matibabu hayo huweza kuwa ya dawa za HOMONI kutegemea na ukubwa wa tatizo pia tiba nyingine ni upasuaji hasa wa kuondoa kizazi kitu ambacho hugharim sana maisha ya mahusiano iwapo mhusika hakuzaa na pia endapo mwanamke atapata tatizo hili akiwa mjamzito basi mimba Yake hutoka na hupata uchungu mapema kabla ya siku ya kujifungua

USHAURI :WANAWAKE WENGI HUWA NA DESTURI YA KUPUUZA KWENDA HOSPTAL KWA KUONA TATIZO NI DOGO HVYO NDUGU RAFIKI HAKIKISHA UNAENDA KUPIMA AFYA YAKO MARA KWA MARA ILI KUWEZA KUTAMBUA MATATIZO MAPEMA HIVYO TUACHE TABIA YA KUPUUZIA KITU HATA KAMA NI KIDOGO
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia email na namba yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA ZA AFYA TEMBELEA BLOG HII
naythamhealthcare.blogspot.com

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email:nsalum998@gmail.com/+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI/PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)

FAHAM UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu zangu ni matumaini yangu mnaendelea vyema kabisa,napenda kuwataka radhi na kuwapa pole Kwa ukimya wangu kutokana na kupisha shughuli za uchaguzi, Nimepokea emails zenu nyingi sana za kunimiss nimefarijika napenda kuwaambia nami NIMEWAMISS NA NINAWAPENDA WOTE pamoja na hayo nimeona emails zenu zinazohusu magonjwa mbalimbali yanayowasumbua wanawake wengi na hivyo Leo hii napenda nianze na ugonjwa wa PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI )

UGONJWA WA PID NI NINI??
~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)

VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID
~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa PID zipo njia kadhaa hatarishi kusababisha maambukizi haya Nazo ni ÷
👉kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi(IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
👉Kufanya ngono isiyo salama
👉Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika
👉Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID
👉Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama

DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni
👉Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
👉Kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
👉Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
👉Kutokwa na hedhi bila mpangilio
👉kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya

VIPIMO NA MATIBABU YA UGONJWA WA PID
Matibabu ya tatizo hili yanapatikana kote nchini kwa kufata misingi ya utabibu kuzingatia majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali ili kuweza kubaini tatizo kwa kufanya vipimo tofauti
MFANO
👉FULL BLOOD PICTURE _kipimo hiki kinatumika ili kuweza kutambua aina  mbalimbali za chembe damu zilizoathiriwa na maambukizi ya PID
👉CERVICAL CULTURE_Hutumika ili kujulia aina ya vimelea waliosababisha PID
👉ULTRASOUND _hutumika kuangalia katika nyonga kama kuna athari yoyote imetokea katika mfumo wa uzazi
~mara baada ya kufanya vipimo na mgonjwa kugundulika kama ameathirika na tatizo hili mara nyingi dawa za antibiotics ambazo ni DOXYCYCLINE,CEFOXITIN,MYCIN,GENTAMYCIN,CLINDAMYCIN,SULBACTAM,AMPICILLIN, huhusika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa huu lakini ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali  ambayo imewekwa na mamlaka na wizara  ya afya kati ya sehem moja hadi nyingine hivyo si ruhusa kujinunulia dawa na kumeza pasipo ushauri wa daktari

NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na  vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉JIWEKEE TABIA YA KUFANYA VIPIMO MARA KWA MARA HASA KIZAZI
👉USIFANYE MAPENZI MARA BAADA YA KUJIFUNGUA AU MIMBA KUTOKA MPAKA UTAKAPOHAKIKISHA SHINGO YA UZAZI IMEFUNGA VEMA
👉KUWAHI KUONANA NA DAKTARI UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA
👉KUWA MSAFI NA KULA LISHE BORA
NOTED:NDUGU RAFIKI UONAPO DALILI ZA UGONJWA HUU WAHI KUPATA MATIBABU KWANI UGONJWA HUU NI MKUBWA HUWEZA KUSABABISHA UGUMBA  IKIWA HAUTAPATA TIBA VIZURI

Kwa makala zaidi za afya tembelea blog yangu hapo chini
naythamhealthcare.blogspot.com

asante kwa kuwa nami kusoma ujumbe huu rafiki kama una MAONI/MASWALI NIANDIKIE KUPITIA NAMBA NA EMAIL YANGU HAPO CHINI PIA TAFADHALI NISAIDIE KUIFIKISHA ELIMU HII KWA WENGINE

Makala hii imeandaliwa na
Dr Naytham
+255623026602/+255746465095
email;nsalum998@gmail.com
naythamhealthcare.blogspot.com
USISAHAU KULIKE,KUKOMENT NA KUSHARE NA RAFIKI ZAKO