BREAKING
BannerFans.com

Alhamisi, 17 Novemba 2016

TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI (OVARIAN CYST)

FAHAMU ATHARI ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST)

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatull,
 Naam natumaini mnaendelea vizuri napenda kumshukuru Mungu kwa kunijaalia Afya kuweza kuandika makala hii inayohusu uvimbe katika mayai ya mwanamke hivyo ungana nami rafiki kupata elimu hii

OVARIAN CYST NI NINI??
~Ni uvimbe unaotokea katika mayai ya mwanamke (ovarian)
~uvimbe huo hutokana na mkusanyiko wa maji maji yanayozungukwa na kutu nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke
~uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa rika tofauti na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofika umri wa kushika ujauzito
~uvimbe huu huweza kuwa na ukubwa wa cm3_cm30 na unaweza kujaza tumbo lote

AINA ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE
(@)HEMORRHAGIC CYST ~hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa Aina yoyote ule ambao umeshajitengeza tayari,pia uvimbe huu huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu (kushoto /kulia)

(@)FOLLICULAR CYST ~hii ni Aina ya uvimbe unaotokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu una ukubwa wa wastani 2:3 kwa upana, uvimbe huu hauna dalili yoyote na hupotea yenyewe baada ya Muda

(@)CORPUS LUTEUM ~hii ni Aina ya uvimbe ambazo unatokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu husinyaa na kupotea wenyewe ingawa wakati mwingine huweza kujaa maji na kusababisha tumbo kuvimba upande mmoja

(@)DERMOID CYST ~uvimbe huu hujulikana kama MATURE CYST TERATOMA, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika ujauzito na uvimbe huu huweza kukua nchi 6 kwa upana na ndani Yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mifupa, mafuta na cartilage, pia uvimbe huu huweza kuwa mkubwa zaidi na kujizungusha hivyo huathiri mzunguko wa damu na hivyo kusababisha maumivu makali ya nyonga na tumbo.

(@)POLYCYSITIC APPEARING CYST ~huu ni uvimbe mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijiuvimbe vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye Afya njema na wale wenye tatizo la homorne

(@)CYSTEDENOMA ~hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea kwenye tissue za ovary na hujazwa na maji maji Aina ya kamasi pia uvimbe huu una ukubwa wa nch, 12 au zaidi kwa upana

(@)ENDOMETRIOSIS ~huu ni uvimbe unaosababishwa na uwepo wa Aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama ENDOMETRIUM kwenye mayai ya mwanamke, uvimbe huu huathiri wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu makali (sugu) ya nyonga (CHRONIC PELVIC PAIN) wakati wa hedhi, pia uvimbe huu una rangi nyekundu ya kahawia (reddish brown) na una ukubwa wa 0.75_8 inches


VIHATARISHI VYA TATIZO HILI
👉kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka (IRREGULAR MENSTRUATION CYCLE)
👉kuwa na mafuta mengi tumboni
👉kukosekana kwa uwiano wa vichocheo mwilini (hormone imbalance)
👉kuvunja ungo mapema yani kuanzia miaka 11kushuka chini
👉kutumia dawa za kemikali maana zina side effects

DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI
👉mwanamke kupata maumivu /kichomi ambayo huwa hayana Muda maalumu huchoma ukeni, kiunoni, mgongoni, mapaja, NK
👉kuhisi tumbo kuwa zito limejaa au kuvimba
👉kupata maumivu makali katika matiti
👉kutopata hedhi katika mpangilio
👉kuongezeka uzito mara kwa mara
👉kupata maumivu katika mbavu
👉kuumwa kichwa mara kwa mara
👉nywele kukua haraka kila wakati
👉kupata maumivu makali wakati wa hedhi
👉kuhisi kichefchef (kutapika)
👉kupata maumivu makali ya nyonga
👉kuhisi uchovu
Kila wakati
👉kutokwa na matone ya damu
👉kutoshika mimba
👉mabadiliko katika upatikanaji wa haja
@haja ndogo kutoka Bila kujielewa
(b) haja kubwa kuwa ngumu

VIPIMO NA MATIBABU
Matibabu hufanyika kwa kuangalia Majibu yaliyopatikana katika vipimo, Kuna vipimo vingi vya kuona tatizo hili kama vile ENDOVAGINAL ULTRA SOUND, COMPLETE BLOOD COULD, SERUM CA 125 ASSAY, URINE FOR PREGNANCY, baada ya daktar kupata Majibu ndio huangalia tiba inayoendana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya Aina mbili

(@)MATIBABU YA DAWA
~tiba hii huhusisha matumizi ya dawa za upangaji uzazi kwa Muda wa wiki 4_6, matumizi ya dawa Hizi kwa Muda mrefu huzuia kutokea tena uvimbe katika kizazi kwasababu dawa Hizi hufanya Kazi ya kuzuia mayai kutotoa mayai ya uzazi (ovums) pia dawa Hizi hazipunguzi uvimbe uvimbe kwasababu uvimbe utapotea wenyewe baada ya Muda

(B) TIBA YA UPASUAJI
~katika tiba hii ya upasuaji Kuna Aina mbili

(1)EXPLORATORY LAPARATOMY
~katika tiba hii mgonjwa hupasuliwa tumboni na daktar huweza kuondoa uvimbe, upasuaji huu hufanyika kwa mwanamke mwenye uvimbe ambao hauwezi kupotea na mkubwa kuanzia 5cm_10cm

(2)LAPARASCOPIC SURGERY
~huu ni upasuaji ambao daktari hupasua sehem ndogo na kutumbukiza mpira maalumu ambao una kamera kwa mbele na huondoa uvimbe katika mayai, upasuaji huu hupendwa na wanawake wengi kwasababu hauachi kovu lolote na mara nyingi hufanyika kwa uvimbe mmoja
NOTED :NDUGU RAFIKI hakikisha unaenda kupima Afya yako mara nyingi kwani Kuna watu wapo na tatizo hili ila wanashindwa kuelewa au hawajitambui hivyo ni bora ukaepuka ugonjwa huu kwani madhara Yake ni kusababisha UGUMBA.
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali, maoni, mapendekezo yoyote niandikie kupitia email  na namba yangu hapo chini

KUSOMA MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA KATIKA BLOG HII NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
email:nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095
PLZ USISAHAU KUSHARE, KUKOMENT, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

Hakuna maoni :