BREAKING
  • FANGASI UKENI

    Pata suluhisho la tatizo la fangasi ukeni pamoja na ushauri utakaokufanya uwe salama daima

  • TIBA YA NGUVU ZA KIUME

    Okoa nyumba yako kwa kupata dawa itakayo ongeza nguvu zako za kiume na kudumisha unyumba daima

  • SULUHISHO LA U.T.I

    Je hauna ufahamu wowote kuhusu U.T.I ?Je Unakabiliwa na tatizo la U.T.I?Wasiliana nami nikujuze zaidi huenda una tatizo la U.T.I lakini haujijui,na kama unalo basi tiba yake ipo

  • TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

    Je Umesumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu pasina kupata suluhisho,wasiliana nami nikupatie dawa itakayoondoa tatizo lako kabisa

BannerFans.com
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo tiba kwa wanaume. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo tiba kwa wanaume. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 13 Mei 2017

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE NA SULUHISHO LAKE

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE NA SULUHISHO LAKE






KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji
Naam ni jambo la kumshukuru Allah kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Allah kwa kila kitu katika maisha yako
Ama baada ya salam Leo ni vyema tukapata darasa kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu

Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.


Kuvimba Tezi Dume (BPH)


Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.


BPH husababishwa na nini?

Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.

Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika

damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye

kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

Dalili za BPH
Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

Hukojoa mkojo unaokatika katika
Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
Husita kabla ya kuanza kukojoa
Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH


Madhara ya BPH
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na


Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
Madhara katika figo au kibofu
Shinikizo la damu
Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
Maambukizi mbalimbali
Nimonia (Pneumonia)
Damu kuganda
Uhanithi
Vipimo na Uchunguzi

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake
kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
Matibabu

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa njia ya dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).
Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa


Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo

Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwaKula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.[Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.

Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta

hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji
Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.


Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.Kutoa mbegu (Ejaculation):

Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra

karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia

kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa mojaIngawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kwa mwezi


Prostasure Capsule




Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata vifuatavyo
Extractum of Radix Rehmanniae, Rhizoma Anemarrhenae, Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus Ligustri Lucidi, Harba Plantaginis, Radix Paeoniae Rubra.

KAZI NA FAIDA YA HII DAWA
Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la tezi dume na inawafaa Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya kujikinga na tezi dume

 Prostasure Inasaidiaje?
Dawa hii inazuia na kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume kama, kukojoa kila mara, mkojo kutoka kwa shida au maumivu wakati wa kukojoa. Prostasure inaboresha mzunguko wa damu na kuzuia ukuaji wa vijidudu wadogo wanaoweza kusababisha maambukizi katika tezi dume

Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zangu za afya nasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE UJUMBE  KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZANGU HAPO CHINI

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI  ZA AFYA TEMBELEA
 NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

 ~Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham Salum
E-mail nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

Jumamosi, 7 Januari 2017

TIBA SAHIHI YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

FAHAMU TIBA YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu mpenzi msomaji  katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote,
 Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa na  Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake,
 
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuna sababu zaidi ya 250 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume,Mtu anaweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo

MAANA YA NGUVU ZA KIUME
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.

Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za  acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi;

2. Uume kusimama kwa uregevu;

3. Kuwahi kufika kileleni;

4. Kuchelewa sana kufika kileleni ( kushindwa kufika kileleni kabisa);

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa;

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo;

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji;

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Mpendwa  msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.

Lakini nini kinachopelekea viungo hivyo vishindwe kufanya kazi vizuri?
Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia).

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua TAHADHARI kabla ya HATARI!

KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI!
Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana!

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo. Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanaume  wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana.

Nani anaweza kutibu nguvu za kiume?
Kuna watu wengi sana hivi leo wanaodai kutibu nguvu za kiume. Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kweli! Ni watu wachache sana wana uwezo wa kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Utakuta mtu anatangaza dawa ya aina moja kuwatibu watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume. Tabia hii pia imejengeka kwa baadhi ya watu, hupiga simu na kuuliza moja kwa moja, "Daktari, dawa za nguvu za kiume ni shilingi ngapi?"

 Kila mwanamume ana sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume. Kama wanaume 100 waliopungukiwa nguvu za kiume watajipanga mstari, kila mmoja atakuwa na sababu yake na chanzo chake cha kupungukiwa nguvu za kiume tofauti kabisa na mwingine.

Hii humaanisha kila mgonjwa atakuwa na dawa yake ya kipekee kabisa tofauti na mwingine. Sasa itashangaza kuona huyu kapungukiwa nguvu za kiume kutokana na mishipa ya ateri kutofanya kazi vizuri, na yule kapungukiwa nguvu kutokana na kuvimba kwa tezidume,Halafu wote wapate dawa aina moja! Hiki ndicho kinachofanyika na watu wengi wamepoteza pesa na muda kwa matibabu yasiyokuwa na maana.

Yahitajika daktari mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo, ndiye anayeweza kutibu tatizo la nguvu za kiume. Yaani, daktari ambaye anajua vizuri ndani na nje utendaji wa figo, ini, moyo n.k; awe ni daktari wa tiba asilia au daktari wa tibakemikali (yaani daktari wa hospitali) siyo kila mtu tu au kila daktari. Hata kama utakwenda kwenye hospitali kubwa yoyote duniani unayoijua, na ukagonga hodi katika chumba cha daktari, ukamwambia, "Nina tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume," atakurifaa kwa daktari maalumu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo. Hata kwa madaktari wa tiba asilia, hali ni hivyo hivyo, lazima ukutane na ambaye amebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Kwa sababu unapotibu nguvu za kiume unakuwa unatibu viungo vya mwili kwa ujumla. Daktari aliye mtaalamu anakuwa ana uwezo wa kutambua tatizo la kiungo kilichokorofisha mwilini kutokana na kumhoji mgonjwa; na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiridhisha kwa vipimo.

LISHE MUHIMU KUREJESHA NGUVU ZA KIUME
wakati mwingine mwanamme hupatwa na tatzo la Nguvu Za Kiume kutokana na kukosa madini lishe muhimu yanayohitajika mwilini mwake
Naam tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.

Antioxidant Nutrients

Upungufu wa vitamin E, vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa (sperm motility). Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa (International Units - IU) 100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza kumzalisha mwanamke (infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba mwanamke. Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye shahawa (sperm count) na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Tafiti pia zimeonyesha kwamba selenium husaidia uogeleaji wa shahawa.

Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA) ya vitamin C ni miligramu 90. Mwanaume anayevuta sigara anahitaji miligramu 125. Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits), cantaloupe, kiwi, maembe, strawberries, broccoli, cauliflower, pilipili nyekundu na juisi ya nyanya. Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source) na 22 (synthetic). Vyakula muhimu ni pamoja na ngano, karanga na jamii zake, mafuta ya mimea, mbegu zisizokobolewa (whole grains). Selenium RDA ni 15 micrograms. Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood, kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga, vitunguu swaumu.

Vitamin B12

Upungufu wa vitamin B12 hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility. Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa zake, mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).

Zinc

Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa. Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc. Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi kidogo cha homoni za kiume (low testosterone levels). Wanaume wenye shida hiyo wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba. RDA ya zinc ni miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8). Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza, dark turkey meat, lentils, ricotta cheese, tofu, yogurt, spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya. Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.

L-carnitine

Husaidia kuongeza sperm count. Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye nyama na maziwa

NOTED;KABLA YA MATUMIZI YA DAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NI VYEMA UKAWASILIANA NA DAKTARI WAKO WA KARIBU ILI KUPATA USHAURI ZAIDI

Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA NAYTHAMHEALTHCARE.BLOGSPOT.COM

Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud
Email-nsalum998@gmail.com
+255623026602/+255746465095

PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUNZA