BREAKING
BannerFans.com

Jumapili, 9 Oktoba 2016

FAHAMU FAIDA 11 ZA KUNYWA MAJI YENYE NDIMU ASUBUHI



HIZI NDIO FAIDA 11 ZA KUNYWA MAJI YA NDIMU ASUBUHI 

 Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, Nina imani mmeamka salama na mnaendelea vyema wapendwa ni jambo la kumshukuru mungu Kwa hakika 

Mpenzi msomaji nina imani umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).

Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.

Faida 1: Huchochea Mmeng’enyo Wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida 2: Huboresha Kinga Za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 Faida 3: Husaidia Unyonywaji Wa Madini Mwilini

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida 4: Husaidia Kinga Dhidi Ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida 5: Husaidia Kupunguza Hatari Ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

Soma pia: Madhara ya kula chumvi nyingi kwa afya ya binadamu

Faida 6: Usafishaji Wa Mwili Na Damu

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

 Faida 7: Kurekebisha Sukari Katika Mwili


Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

Faida 8: Dawa Ya Kikohozi Na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

Faida 9: Inasaidia Urekebishaji Wa Ngozi Na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.

Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

 Faida 10: Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

 Faida 11: Kuondoa Harufu Ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

 Anza Siku Kwa Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Siku,
Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.
 NB :HAIFAI KWA WENYE VIDONDA VYA TUMBO 
  
 Asante Kwa kuwa nami kupata elimu hii mpenzi msomaji kama una swali au maoni unaweza kuniandikia ujumbe kupitia namba na emails yangu hapo chini 

Kwa makala zaidi za afya naomba utembelee blog yangu ya 
Naythamhealthcare.blogspot.com 

makala hii imeandaliwa na Dr Naytham S Masoud 
email nsalum9998@gmail.com
0689538628

  
TAFADHALI SHARE NA WENGINE WAPATE KUJIFUNZA ELIMU HII

Hakuna maoni :